24.7 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Waziri Nape: Lengo tutengeneze sheria itakayodumu

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Wakati Wadau wa Habari wakiendelea kutoa elimu kuhusu mapendekezo ya Sheria ya Habari yaliyowasilishwa Serikalini, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema kwa hatua iliyofikiwa wadau wanafuraha nakwamba lengo ni kutengeneza sheria ya kudumu.

Waziri Nape ameyasema hayo leo Jumatano Julai 13, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akifungua mkutano wa Wadau wa Maendeleo ambapo amesema kuwa Serikali imepokea maoni nayo ikatoa yakwake juu ya kuboresha tasnia ya Habari.

“Kwa hapa tulipofika wadau wana furaha, hata ukiwaita na ukiwauliza. Wameleta maoni yao nasi tumetoa ya kwetu, tumejadiliana ili kuona namna ya kuboresha.

“Sheri ya Habari ilipotungwa, ililenga kutakua matatizo ya habari ikiwemo matatizo ya ajira zao, maslahi yao, mazingira yao ya kazi, haki zao na wajibu wao. Sasa inawezekana masuluhisho yaliyopo kwenye sheria, ndio yanayogombaniwa kwamba ni sahihi ama si sahihi,” amesema Waziri Nape.

Katika hatua nyingine Nape amesema kuwa serikali imetoa nafasi kwa wanahabari kupeleka mbadala wa yale yanayolalamikiwa.

“Katika mazingira hayo, serikali imetoa nafasi kwa wanahabari kuleta mbadala wa yale yanayolalamikiwa, tukae mezani tuzungumze na huo mchakato haiwezi kuwa mfupi, ni chakato wa mazungumzo mie nimeukuta na tuaendelea nao. Tuna malengo ya kuukamilisha mapema kadri inavyowezekana.

“Lengo tutunge sheria itakayokaa muda mrefu lakini sheria itakayokubalika na pande zote mbili lakini itakayotengeneza mazingira kuwa bora zaidi kuliko tuliyonayo,” amesema Nape.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles