25.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 30, 2024

Contact us: [email protected]

TPDC yajivunia kuongoza kwa ulipaji kodi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC) limesema linajivunia kuwa shirika la umma linaloongoza kwa ulipaji kodi.

Akizungumza katika Maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara sabasaba, Afisa Uhusiano wa TPDC, Francis Lupokela amesema ulipaji kodi kwa wakati umewawezesha kushiriki maonyesho hayo ili kuwaonesha wananchi kazi zinazofanywa na shirika hilo.

Amesema asilimia 62 sawa na megawat 1,021.32 ya umeme unaotumika nchini unatokana na gesi asilia jambo hatua ambayo amesema kuwa ni ya kujivunia kwa taifa.

“Tunajivunia kuwa walipaji wakubwa wa kodi kama shirika tunawaomba wananchi waje wajifunze waone kazi kubwa inayofanywa na shirika lao na siyo kuogopa,” amesema Lupokela.

Amesema kwa sasa shirika limesimamia miradi mikubwa mitatu ambayo ni pamoja na mradi wa Eyasi Wembere ambao ni mradi wa mafuta na gesi asilia, bomba la mafuta Eacop na gesi asilia ya LNG.

Amesema kwa sasa nyumba 1,500 zinatumia gesi asilia viwanda 48, Taasisi za Kiserikali 2 gereza la keko na chuo kikuu cha Dar es Salaam.

“Mbali na nyumba hizo TPDC pia inatoa huduma ya gesi asilia kwa Serena Hoteli na taasisi nne za serikali ziliopo Mtwara,” amesema Lupokela.

Amesema zaidi ya magari 1,400 hapa nchini yanatumia gesi asilia.

Aidha, ameiomba serikali kuendelea kuliamini shirika hilo katika suala zima la ufanyajikazi na kwamba lishirika hilo lipo kwa ajili ya kuipa heshima na hadhi nchi katika kukamilisha miradi kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles