24.4 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Dk. Biteko atoa siku saba kwa wachimbaji kulipa madeni ya wananchi Bahi

Na Mwandishi Wetu, Bahi

Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko, ametoa wiki moja kwa wachimbaji wa madini ya Chuma wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma kulipa madeni wanayodaiwa na wananchi katika migodi hiyo kwa wanaofanya kazi ya kuponda madini hayo.

Agizo hilo amelitoa Julai 4, 2022 wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Asanje mara baada ya kutembelea maeneo ya wachimbaji wa chuma na kupokea malalamiko.

Dk. Biteko, amemwelekeza Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Dodoma kusimamia agizo hilo kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda ili wanachi hao wa Asanje walipwe fedha zao wanazowadai wawekezaji hao.

“Mhe Mkuu wa wilaya, kama kuna mtu atakuwa hajalipwa hadi jumatatu Afisa Madini unasimamisha mgodi huo mara moja bila masharti yoyote, uandike kabisa kwa maelekekeao ya Waziri nasimamisha,” amesisitiza.

Aidha, amewataka wachimbaji wa madini na wawekezaji katika Sekta ya Madini kuhakikisha wanashirikisha wananchi katika mipango yao ya uwekezaji kabla hawajawekeza kwenye miradi hiyo ili kupunguza malalamiko yanayojitokeza mara kwa mara.

Amesema, ushirishwaji utasaidia kujua vipaumbele vya wanachi ili iwe rahisi kwa utekelezaji.

“Nataka niwaambieni wenye leseni, leseni hizi mmepewa kwa niaba ya Watanzania wengine. Kwa kuwa tumewapa wenzetu leseni ya kuchimba matarajio ya Serikali ni kwamba hawawezi kugeuka tena kuwa kero kwa watu ambao wako maeneo ya kuchimba,”amesema.

Nae, Mbunge wa Jimbo la Bahi, Kenneth Nolo amesema, ziara ya Dk. Biteko katika Kijiji cha Asanje kusikiliza malalamiko ya wanachi hao, imekuwa na manufaa kwa wananchi na matarajio makubwa katika shughuli za uchimbaji madini.

Katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Munkunda amemshukuru Dk. Biteko kwa kuweza kufika na kusikiliza changamoto za wananchi hao kwani ilikuwa ni kiu kubwa ya kuweza kufikisha malalamiko yao kwake.

Wilaya ya Bahi yanapatikana madini mbalimbali yakiwemo dhahabu, chuma na madini ujenzi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles