31 C
Dar es Salaam
Thursday, December 19, 2024

Contact us: [email protected]

Simu ya Infinix 11 Series yazinduliwa Tanzania

Na Beatrice Kaiza, Mtanzania Digital

Kampuni ya Tigo Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu ya Infinix Tanzania wamezindua simu mpya ya Infinix NOTE 11 Pro, ambayo itapatikana kwenye maduka ya Tigo na Infinix nchini kwa bei ya 600,000 na NOTE 11 kwa Shilingi 510,000.

Akizungumza na Wanaandishi wa Habari, jijini Dar es Salaam leo Alhamis Novemba 11, kaika Uzinduzi huo Meneja wa Bidhaa za Intaneti kutoka Tigo, Mkumbo Myonga amesema lengo nikuwaunganisha wateja wao.

“Kama kawaida yetu tunaendelea kuwaunganisha wateja wetu katika huduma za Kidigitali na leo kwa mara nyingine tena kwa kushirikiana na wenzetu wa Infinix kuwaletea Infinix NOTE 11 Series, simu bora kabisa ambayo utarahisisha ukuaji wa huduma za Kidigitali na Intaneti nchini, na tunawashukuru washirika wetu Infinix Tanzania kwa kuendelea kuamini njia zetu za usambazaji wa kina, mtandao mpana wa 4G, na msingi wa wateja wetu ambao unatafsiri mauzo ya kifaa cha hali ya juu kilichozinduliwa.

“Mkakati wetu ni kuhakikisha usambazaji wa simu janja kote nchini huku tukihakikisha wateja wanafurahia matumizi bora ya huduma za Kidigitali kupitia Mtandao wa kasi zaidi wa 4G+ ambao ni mkubwa zaidi nchini, tunatoa GB 96 za Intaneti BURE kwa mwaka mzima,” amesema Myonga.

Kwa upande wake Afisa Mahusiano kutoka kampuni ya Infinix, Aisha Karupa ameongezea kuwa mfululizo wa INFINIX NOTE 11 umewekwa ili kukidhi mahitaji ya kila mtumiaji ndani ya mazingira yake ya kazi na hivyo Infinix inaleta nguvu ya haraka, nguvu ya ufanisi zaidi na utendaji unaotumia mchanganyiko wa kipekee wa teknolojia ya hali ya juu na kwa bei nafuu.

“Infinix NOTE 10 PRO ni moja kati ya simu janja ya kwanza nchini kuwa na tekinolojia ya Mediatek’s Helio G 96 ambayo inarahisisha katika suala zima la kucheza Games, Processor ya 120 Hz 6.95’FHD + Camera Bora kabisa na Betri yenye uwezo wa kukaa na Chaji kwa Muda Mrefu, tunawakaribisha wateja wetu wote katika maduka ya Tigo na Infinix kote nchini waweze kujipatia simu hizi mpya kabisa zilizoambatana na Ofa kibao,”amesema Aisha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles