Renatha Kipaka, Bukoba
Wanafunzi wa kidato cha Nne wanaotarajiwa kufanya mtihani wao wa kuhitimu Jumatatu ya Novemba 15, 2021 wameaswa kufuata mafundisho bora waliyoyapata shuleni na kusimama katika kutenda mema katika jamii.
Ushauri huo umetolewa na Khadija Jamal Karumuna ambaye nimtahiniwa wa Kidato cha nne katika shule ya Sekondari Kemebos iliyoko mkoani Kagera wakati wa mahafali yaliyofanyika shuleni hapo.
Amesema mwanafunzi awapo shuleni anafundishwa mambo mengi ya maisha, hivyo baada ya kuhitimu masomo yetu tunatakiwa kuwa makini na kuepuka vishawishi.
Amesema elimu ya kidato cha nne iwe sehemu ya ufunguo kwenye maisha ya kila siku, wapo walitamani nafasi hii hawakuweza kufanikiwa kwa sababu mbali mbali
“Niseme tu kwa jinsi tulivoandaliwa darasani na hata nje ya darasa inatosha kabisa kuepuka vikwazo na kufanya mema na mafundisho ya pande zote mbili wazazi na walimu,”amesema Jamali.
Ameongeza kuwa, Tsdcfaifa linathamini maendeleo na ukuwaji wa uchumi kupitia elimu ambayo inafundishwa shuleni kuna asilimia kubwa na kuheshimiwa.
Meneja wa shule hizo, Eurogius Katiti amesema, Taasisi ya Kaizirege na Kemebos imeweka uimara katika kujenga, Misingi ya vijana kwa kuwaanda kuwa wataalamu wa badae.
Amesema taasisi hiyo imeandaa mafunzo ya sayansi na biashara hivyo itasaidia kuwapo na wataalamu ambao watakuza uchumi wa nchi.
“Kuwapo kwa Taasisi hiyo imesaidia sana wanafunzi katika kufundisha sayansi ya Jamii na biashara ikiwa ni kuimarisha wataalamu ambao wataendeleza sekta hizo,” amesema Katiti.
Naye Mgeni Rasmi katika mahali hayo, ambae ni Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Bukoba, Jacton Rugumila alisema taifa linahitaji watu wenye ubunifu na wenye kupunguza garama za kuagiza vifaa nje.
Amesema kwa kutumia wataalamu wa ndani itarahisisha kupunguza garama ya kutengeneza vitu, kwani wataalamu wanaandaliwa kwenye shule zetu.