26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Shule za Atlas kuja na mbio za Marathon kusadia wanafunzi waliofiwa na Wazazi wao

Na Brighiter Masaki, Mtanzania Digital

Katika kuhakikisha Mtoto anapata elimu bora, Uongozi wa Shule za Atlas zimeandaa mbio zitakazohusisha zaidi ya watu 2,000 ili kusaidia kulipia ada za wanafunzi waliopoteza wazazi wao wakati wa mlipuko wa Uviko-19.

Mbio hizo zitajulikana kama Atlas School Half Marathon 2021 zinatarajiwa kuanza Oktoba 14, mwaka huu zikihusisha mbio za Km 21, 10 na Km 5.

Katika kufanikisha mbio hizo, Atlas wamekuja na Kauli mbiu inayosema ‘Kimbia kizalendo changia elimu kwa watoto wasiojiweza’.

Akizungumza jana kuelekea mbio hizo, Mkurugenzi wa shule za Atlas, Sylivanus Rugambwa, amesema baada ya shughuli ya marathon kukamilika watakuwa na sherehe za mahafali ya 19 ya shule zao za msingi Atlas Madale na Ubungo, Atlas Sekondari na Shule za awali.

“Tunategemea kuwa na idadi kubwa ya watu zaidi ya elfu kumi na tano ambao watashiriki katika mahafali hayo katika kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa kamati imejiandaa vyema pamoja na watendaji wake ili kunogesha sherehe hiyo za mahafali na marathon,” amesema.

Amesema lengo kubwa la kufanya mbio hizo ni kuchangia watoto wanaosoma katika shule hiyo ambao wazazi wake walifariki kuanzia mwaka jana kutokana na ugonjwa wa Uviko-19.

Rugambwa amesema, hawataki kuona watoto hao wanakosa elimu bali wanahitaji kuendelea kusoma na kupata elimu bora katika kipindi hiki ambacho wamepoteza wazazi wao.

Aidha, ameongeza kuwa katika kuhakikisha mbio hizo kamati ya utendaji imeandaa siku ya jumamosi kuanzia saa 12 asubuhi siku ya ukaguzi wa njia ya wakimbiaji ambao watapenda kushiriki watakagua pamoja na njia ya Km 5, Km 10 na Km 21 itakayotumika siku ya Atlas Half Marathon.

Ameongeza kuwa katika mbio hizo mgeni ramsi anatarajiwa kuwa Waziri Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe sambamba na wageni mbalimbali katika mbio hizo.

“Tunategemea mbio zetu zitahughuliwa na watu mbalimbali wakiwemo wazazi,watoto,wanafunzi mbali mbali wakimbiaji nguli,wakimbiaji wa kawaida pamoja na makundi maalum,watu mashuhuri viongozi wa serikali,” amesema.

Rugambwa amesema, kuwa zoezi la usajili wa mbio hizo bado unaendelea katika shule zao za Madale na Ubungo kwa kulipia namba 5927380 pamoja na kituo cha Mlimani City kuanzia saa 2 asubuhi na jioni ya saa 12.

Hata hivyo katika mbio hizo mshindi wa kwanza katika mbio za Km 21 Sh 350,000 , kilometa 10 Sh 200,000 na Km 5 Sh 100,000.

Aidha, mshindi wa pili ni KM 21 ni Sh 300,000, Km 10 Sh 175,00 Km 5 Sh 75,000 huku mshindi wa tatu ni Km 21 Sh 200,000 Km 10 Sh 150,000 na Km 5 Sh 50,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles