31.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 15, 2024

Contact us: [email protected]

Azam FC yapigwa na Polisi

Na Daines Msumeno,TUDARCo

Timu ya Azam FC imepoteza mchezo mbele ya maafande wa Polisi Tanzania ikifungwa mabao 2-1 katika mechi wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliopigwa kwenye dimba la Ushirika, mjini Moshi.

Azam inakosa ushindi katika mchezo wa pili wa ligi hiyo baada ya ulioopita kutoka sare ya 1-1 na Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha Msaidizi wa Azam, Vivier Bahati, amesema matokeo hayo si mazuri kwao, wamefanya makosa katika safu ya ulinzi.

“Tumepata nafasi lakini wachezaji ni kama walikuwa na presha na walikuwa wanakimbia na mpira wanafanya maamuzi yasiyo sahihi, ndiyo tumepoteza kwa staili hiyo,” amesema Bahati.

Mchezo mwingine uliomalizika saa 10:00 jioni ya leo, Coasta Union imelazimishwa sare na KMC Uwanja wa Mkwakwani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles