25.1 C
Dar es Salaam
Thursday, December 5, 2024

Contact us: [email protected]

Dodoma Jiji Fc yapata udhamini mnono 10BET

Na Ramadhan Hassan,Dodoma 

KLABU  ya Soka ya Dodoma Jiji inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) imeingia makubaliano ya  udhamini wa miaka mitatu na kampuni michezo ya  kubashiri Barani Afrika ya  10BET.

Hafla ya makubaliano hayo, uliokwenda sambamba na utambulisho wa jezi za msimu wa 2021/2022 za timu hiyo, umehudhuriwa na madiwani wa Jiji la Dodoma,wakiongozwa na Naibu Meya  Emmanuel Chibago,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Jabir Shekimweri.


Pia alikuwepo Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini,Anthony Mavunde pamoja na mashabiki wa timu hiyo.  

Akizungumza wakati wa utambulishaji wa kampuni hiyo leo Septemba 27,2021 Jijini Dodoma,Katibu Mkuu wa timu ya Dodoma Jiji, Fortunatus John amesema kupitia makubaliano hayo kampuni hiyo kwa msimu wa kwanza ndio itakayogharamia vifaa mbalimbali vya michezo vitakavyotumika katika mazoezi na mechi.

“Uongozi wa 10BET unaamini  klabu yetu itakuwa  ni mshirika mzuri kwao  na mkataba huu utasaidia kuwafikia mamilioni ya wateja  kirahisi,”amesema.

Kwa upande wake,Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini,Shekimweri amelitaka benchi la ufundi kuendana na uwekezaji ambao uongozi wa timu hiyo umekuwa ikiufanya kwa kuhakikisha timu inapata matokeo katika michezo yake.

“Huu ni uwekezaji mkubwa malengo yetu sisi sasa ni kuwa katika ‘Top 2’ hapa hakuna Usimba wala Uyanga,Dodoma Jiji Fc kwanza, hivyo benchi la ufundi ni lazima liufanyie kazi uwekezaji huu katika matokeo kwa timu kufanya vizuri,”amesema.

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini, Mavunde amesema Dodoma Jiji kwa sasa wamejipanga na hakuna timu ambayo itatoka katika Uwanja wa Jamhuri ambapo ametoa rai kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi viwanjani kuishangilia timu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles