28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

NGO’s zatakiwa kufuata Sheria Arusha

Na Mwandishi Wetu, Arusha

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Arusha, Dk. Athuman Kihamia, ameyataka Mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO’s), katika Halmashauri ya Jiji la Arusha kufuata sheria, kanuni na taratibu pindi wanapotekeleza majukumu yao.

Dk.Kihamia ameyasema hayo jana jijini hapa wakati akifungua maonyesho ya kwanza ya NGO’s zilizopo ndani ya halmashauri hiyo.

Alisema kuwa mashirika hayo yamekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia makundi mbalimbali katika jamii ila lazima yahakikishe yanazingatia kanuni,sheria na taratibu zilizopo.

“Lazima mfuate sheria kanuni na  taratibu kusiwe na kitu kingine nyuma ya pazia ikiwemo kuwa na matumizi sahihi ya fedha lengo likiwa ni kuchochea maendeleo,”alisema 

Dk.Kihamia aliwataka wadau hao wa maendeleo kuendelea kuunga mkoni juhudi za serikali ambazo zimejikita katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi,endeleeni kutumia weledi katika kuwahudumia wananchi.

Kwa upande wake  Mratibu wa Mashirika yasiyo ya kiserikali halmashauri ya jiji la Arusha, Fatuma Amir,alisema katika jiji hilo yapo mashirika yasiyo ya kiserikali 91 ila kati ya hizo asasi 51 ndizo zimeshiriki maonyesho hayo.

Alisema lengo la maonyesho hayo yenye kauli mbiu “Kuimarisha mchango wa NGO’s kwa maendeleo ya taifa,asasi za kiraia zinachangia kuweka mchango wa maendeleo kwa wananchi” ni kwa ajili ya kusaidia jamii kufahamu pindi wanapohitaji huduma mbalimbali kutoka kwenye mashirika hayo.

Mratibu huyo alisema mashirika hayo yanahudumia jamii katika makundi mbalimbali ikiwemo watoto,wanawake,vijana,mazingira,kutoa msaada wa kisheria na uwezeshaji wananchi kiuchumi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Shirika la Emayani Foundation, Wakili Sylvia Mwanga, alisema wanatarajia katika maonyesho hayo ya siku tatu wataweza kukutana na kutoa elimu kwa wananchi wengi.

Alisema shirika hilo linalojihusisha na uwezeshaji wanawake kiuchumi,haki za binadamu na utetezi humu kundi la watoto wakitoa elomu ya ukatili wa kijinsia.

“Katika maonyesho haya tunaelimisha jamii hasa wanawake waliopo mwenye vikundi tunawapa elimu ya kuanzisha biashara endelevu na kuhakikisha wanapaki bidhaa zao katika mazingira ambayo watapata soko nje ya nchi.

“Tunafanya kazi hizi kutokana na changamoto tunazoziona kwenye jamii mfano kundi la wanawake wengi wanaanzisha biashara nzuri ila wengi zinaishia kuwa biashara ndogo hazikui,sisi tunakuja kama shirika kuwapa elimu za biashaar ambazo zitawafanya wakue na kuchangia uchumi wa taifa,”aliongeza

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles