Na Sheila Katikula, Mwanza
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Amina Makilagi ameipongeza taasisi isiyo ya kiserikali ya The Desk & Chair Foundation iliyopo jijini hapa kwa kuonyesha upendo kwa kutoa misaada mbalimbali ya kijamii ambayo imesaidia kutatua changamoto tofauti za kijamii.
Amina ametoa pongezi hizo jana wakati akipokea msaada wa madawati 348 yaliyotolewa na taasisi hiyo kwa lengo la kupunguza uhaba wa madawati kwenye shule mbalimbali wilayani hapa na kusisitizani vyema taasisi na makampuni kuiga mfano wa The Desk & Chair Foundation.
Alisema serikali inatambua juhudi zinazofanywa na taasisi hiyo ikiwemo kuwakatia bima za afya watu wenye mazingira magumu, kutoa taa za sola kwa wanafunzi, kufunga taa za sola kwenye nyumba 420 za nyasi vijijini, kugawa baiskeli 600 kwa watu wenye ulemavu, kujenga madarasa.
Hata hivyo amewataka wananchi ambao walipewa fedha za mkopo wa bila riba na taasisi hiyo kurekesha ili na wengine waweze kunufaika na mradi na kuufanya ubakie kuwa endelevu.
Naye Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sibtain Meghjee amesema madawati hayo yamefadhiliwa na familia mbili wazaliwa wa Mwanza wanaoishi Uingereza na Canada ambao ni familia ya marehemu Mzee G.B Damji.
Amesema familia hiyo imekuwa ikifadhili mambo mengi haswa kwenye elimu kwani siku za nyuma walijenga madarasa,vyoo na kutengeneza madawati Kibara mkoani Mara ambako waliishi kama Meneja wajenery ya Kibaha.
“Familia ya marehemu Andani ambayo ilikuwa ikiishi Malampaka ndiyo walifadhili madawati 200 kati ya haya 348 ya leo. Tunaomba madawati 50 ukabidhi kwa shule ya shule ya msingi Holy Face la jimbo kuu katoliki la Dodoma, na madawati 40 tulikabidhi siku ya mwenge kwenye shule ya Balale na madawati 25 tunakabidhi leo kwa madrasati Fisabillilahi iliyopo wilayani Ilemela,” alisema.
Aliongeza kuwa mwaka 2020/2021 taasisi hiyo imesaidia wanafunzi zaidi ya 10000 washule za msingi na sekondari wa elimu maalum na elimu ya juu kwa kutoa vifaa mbalimbali ikiwamo vitabu,madaftari,rim,kaluleta, sare za shule.
“Hadi hivi sasa tumeweza kufadhili zaidi ya wanafunzi 300 wa masomo ya vyuo vikuu na kozii maalum takribani kwa asilimia 40 ya wanafunzi kwani wamemaliza masomo yao na kuanza kulitumikia jamii. Taasisi hiyo imefadhili ujenzi wa madarasa 12 yaliyoharibika kwenye shule mbalimbali za msingi yakiwamo.madarasa mawili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum ambayo yanakuwa na madawati, vyoo, jiko na bafu.
“Tumefanikiwa kufadhili madawati zaidi ya 4000 kwenye shule za msingi na sekondari za kanda ya ziwa na visiwani lengo ni kuhakikisha wanafunzi wanasoma kwenye mazingira bora,” amesema.
Hata hivyo alisema taasisi hiyo ilianzisha mradi wa kukopesha mitaji midogo midogo ya bila riba kwa wanafunzi wa elimu ya juu na baadhi ya watu kukataa kurejesha mara baada ya kukopa na kupelekea kufeli kwa sababu ya wakopeshwaji kutorudisha mikopo hiyo kwani kitengo hicho kufungwa rasmi.
Naye Afisa Elimu wa Maalum jijiniwa Mwanza, Peter Ndomondo aliishukru taasisi hiyo kwa kutoa msaada huo wa viti na meza yatapelekwa kwenye shule zenye mahitaji maalum wenye ulemavu tofauti tofauti za zilizopo jijini hapa.