WAZIRI Mkuu wa Japan, Yoshihide Suga, amesema hatagombea katika uchaguzi ujao, ikimaanisha ataachia wadhifa huo alioushikilia tangu mwaka jana.
Suga mwenye umri wa miaka 72, aliingia madarakani kukalia kiti cha Shinzo Abe aliyefikia uamuzi wa kujiuzulu na uamuzi wake huu unakuwa wa kushitukiza kwa walio wengi.
Hatua hiyo ya kujiweka kando inakuja huku Japan ikiwa kwenye kiwango cha juu cha maambukizi ya virusi vya Corona, ambapo tayari watu walioambukizwa ni zaidi ya milioni 1.5.
Hivi karibuni, Serikali ya Japan ilikumbana na ukosolewaji mkubwa kutoka kwa raia walioamini kufanyika kwa michuano ya Olimpiki kungeongeza kasi ya maambukizi.