29.9 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mkirikiti aagiza Halmashauri Rukwa kukamilisha miradi

Na Mwandishi wetu, Rukwa

Halmashauri za Mkoa wa Rukwa zimetakiwa kutumia fedha za Serikali Kuu na makusanyo ya ndani kukamilisha miradi ya maendeleo kwa kuzingatia thamani ya fedha, ikiwamo ujenzi wa shule, hospitali na miradi ya maji katika ubora.

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Joseph Mkirikiti, wakati alipofanya ziara ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo katika  Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ikiwa na lengo la kufuatilia utekelezaji wa kazi za Serikali tangu alipoteuliwa kuongoza mkoa  huo.

“Sasa Serikali imepunguza mzigo kwa halmashauri kwa kulipa posho za madiwani hivyo tunategemea kuona fedha iliyokuwa ikilipwa kwao ikitumika kukamilisha miradi ya maendeleo kwenye kata na vijiji,“amesema Mkirikiti.

Mkirikiti ambaye aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Sebastian Waryuba, wakiwa kwenye mradi wa ujenzi wa shule mpya ya kata kijiji cha Kalumbaleza walijionea madarasa sita yaliyofikia hatua ya renta kwa gharama ya sh 11.5 milioni ikiwa ni nguvu za wananchi.

Ameagiza Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga kubadili utaratibu na kukamilisha ujenzi wa shule moja kwa wakati badala ya kwenda na miradi yote.

“Halmashauri wekeni kipaumbele kukamilisha ujenzi wa maboma ya shule zote tano kabla ya Desemba mwaka huu kwa kuanza na shule moja kila mwezi, hivyo viongozi  kazi yenu ni kuhamasisha na kuwatambua wadau na wananchi ili wachangie nguvu na rasilimali fedha kukamililisha ujenzi huo” amesema Mkirikiti.

Katika ukaguzi wa mradi wa maji uliogharimu sh 102 milioni, amebaini  tatizo la uharibifu wa mazingira kwenye chanzo cha maji ambayo ni safu za milima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles