28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, June 6, 2023

Contact us: [email protected]

Makanisa Bukoba yatakiwa kuzingatia taratibu za corona

Na Renatha Kipaka, Bukoba

Makanisa mbalimbali katika Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera yametakiwa kuzingatia taratibu za afya zinazotolewa na wataalamu zitakazo saidia kujikinga na magonjwa ikiwemo corona.

Wito huo umetolewa na juzi mjini humo na Askofu wa Kanisa la Hema ya Ukombozi, King James, wakati alipokutana na Waandishi wa Habari.

Hata hivyo, Askofu huyo amesema kuwa katika Kanisa la Hema ya Ukombozi wameendelea na hatua za kujikinga na mlipuko wa corona kwa kuepusha mikusanyiko ya muda mrefu na kunawa mikono.

“Niseme tu watu tujenge tabia ya kuwa wasafi muda wote kwa kuoga na kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni.

“Sisi kanisani tumeweka mifumo ya madiaba yanayotiririsha maji pamoja na kufanya ibaada zetu kwa muda mfupi ili watu wawe salama,” amesema Askofu James.

Askofu huyo ameongeza kuwa kabla ya mlipuko huo walikuwa wanafanya ibaada zetu kwa masaa saba lakini sasa wamepunguza kutoka masaa sita hadi matatu.

Emiriana Kamugisha ambaye anaishi jirani na kanisa hilo amesema kuwa kutokana na kanisa hilo kuwa na waumini wengi ingekuwa changamoto kama wao wenyewe wangekuwa hawachukui tahadhari.

“Naona wanazingatia usafi kunawa mikono pamoja na kuvaa barakoa hilo limekuwa likinipa imani kuwa wako salama…. hata uvaaji wa barakoa unazingatiwa vizuri kwa kila muumini,” amesema Emiriana.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Meja Jenerali Charles Mbuge Julai 23, mwaka huu akitoa tamko la Serikali kwa wananchi juu ya kutokuwa na mikusanyiko isiyo ya lazima, alisema endapo kuna umuhimu wa kuwapo na shughuli za kijamii lazima lazima ionbewe kibali. Alitaja maeneo ya misiba, yanaweza kuwa na mikusanyiko na kushindwa kujikinga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,307FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles