24.7 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Umeme vijijini wamkosesha usingizi mbunge Ludewa

Na Elizabeth John, Njombe

Mbunge wa Ludewa mkoani Njombe, Joseph Kamonga amesema suala la Vijiji 20 kukosa umeme katika jimbo hilo linamkosesha usingizi.

Kamonga ameyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Lubonde ambapo amesema suala la umeme limekua changamoto kubwa na kwamba wananchi hao wanapaswa kupata umeme kwa kuwa si anasa bali ni maendeleo.

‘’Wananchi wanahitaji umeme wa uhakika, mradi wa uzalishaji unaomilikiwa na kampuni ya Madope Hydro Power watu wa Tanesco wakipita pita wanajua sisi tayari tunao umeme lakini bado hautoshelezi kwa sababu ni wa mgao.

’’Najua mnahitaji umeme hii ni kutengenezewa ajali ya kisiasa si ndio jamani? kwa sababu wananchi watakuchukia sana kwenye vijiji vyote 20 hili jambo hata mimi linaninyima usingizi, ninahangaika usiku na mchana kushirikiana na Diwani wenu kuhakikisha kwamba wananchi wa kata hizi wanapata umeme wa uhakika,’’amesema Kamonga.

Awali, wanachi wa kata ya Lubonde walimuomba mbunge huyo kuwaletea nishati ya umeme ya uhakika ili aweze kufanya shughuli za kimaendeleo.

‘’Tunakuomba mbunge na sisi tuletewe umeme mbona sehemu nyingine kuna umeme wa uhakika, tunashindwa kuwa miradi ya kiuchumi kwa sababu hakuna umeme wa uhakika,usiku unakuwepo mchana hakuna,’’alisema Philiph Kitulile.

Nay, Grace Ngailo alisema changamoto ya kukosekana umeme wa uhakika ni kubwa ambapo tatizo hilo linakwenda hadi kwenye zahanati zao.

‘’Sehemu kama zahanati kukosa umeme wa uhakika hii si sawa tunakua kama tupo nchi nyingine, tunamuomba mbunge wetu akaendelee kulisemea wananchi tunahitaji umeme,’’alisema Grace.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles