30.3 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mahaka Kuu yabatilisha hukumu ya viongozi 9 wa Chadema Tanzania

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mahakama Kuu ya Tanzania leo imetengua hukumu ya Mahakama ya Kisutu Ijijini Dar es Salaam, iliyowatia hatiani viongozi tisa wa Chama Kikuu cha Upinzani nchini (CHADEMA).

Machi mwaka huu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwatia hatiani viongozi hao, wakiongozwa na Mwenyekiti wake, Freeman Mbowe kwa makosa 12 kati ya 13 ambayo walishtakiwa nayo Februari 2018.

Makosa hayo ni pamoja na kuitisha maandamano bila kibali na kusababisha vurugu. Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na viongozi wenzake walitakiwa kulipa faini ya Sh milioni 350 za Tanzania ambazo ni sawa na dola 13,000.

Mbowe na wenzake walikata rufaa na sasa mahakama kuu imeamuru kurejeshwa kwa fedha hizo.

Wakili wa Chadema, Peter Kibatala amenukuliwa akisema wameanza kudai fedha hizo: “Tumeanza mchakato wa kudai faini, lakini wateja wangu rekodi zao zimefutwa leo,” amenukuliwa Wakili Kibatala.

Mbali na Mbowe, viongozi wengine walionufaika na hukumu hiyo ni katibu Mkuu wa Chama hicho, John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Zanzibar ambaye alikuwa mgombea mwenza urais katika uchaguzi mkuu uliopita, Salum Mwalimu.

Wengine ni Halima Mdee, Esther Bulaya, Esther Matiko ambao ni wabunge na waliokuwa wabunge katika bunge lililopita, John Heche na Peter Msigwa.

Mwingine aliyenufaika ambaye hakuwa amekata rufaa ni aliyekuwa Katibu mkuu wa Chadema, Dk. Vicent Mashinji aliyehamia (CCM) na sasa ni Mkuu wa Wilaya ya .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles