Na Mwandishi Wetu, Dodoma
Serikali kwa kushirikiana na wadau inaendelea na mapambano ya kutokomeza vitendo vya ukatili na mauaji ya Wazee kwa kuongeza msukumo na kuimarisha uratibu wa utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Mauaji ya Wazee kwa kipindi cha miaka mitano (2018/2019-2022/2023).
Hayo yumesemwa jijini hapa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mwanaidi Ali Khamis wakati akizungumza na wazee katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee inayooadhimishwa kila Juni 15.
Naibu Waziri Mwaidi amesema kuwa kutokana na vitendo vya ukatili na mauaji ya wazee pamoja na changamoto nyingine zinazoambatana na uzee ikiwemo hofu na wasiwasi, msongo wa mawazo, sononi, upweke, unyanyapaa na magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ambukiza hivyo serikali katika mapitio ya Sera ya Wazee ya mwaka 2003 serikali imeweka msisitizo zaidi katika kuhakikisha wazee wanapata huduma ya msaada wa kisaikolojia na ushauri nasaha ili kusaidia kuimarisha afya na ustawi wao.
“Kwa mujibu wa mwongozo wa Kitaifa wa Utoaji wa Huduma za Msaada wa Kisaikolojia wa Mwaka 2021, matatizo mengi ya kiafya na kimahusiano yanayowakabili wazee yanatibika kikamilifu kupitia msaada wa kisaikolojia na ushauri nasaha,” amesema lisema Niabu Waziri Mwanaidi
Ameongeza kuwa katika kumlinda Mzee kupitia Mpango wa serikali wa kuboresha huduma za afya, Serikali imeendelea kuhakikisha kuwa kila kituo cha Afya cha serikali na Hospitali zinakuwa na madirisha maalum kwa ajili ya matibabu kwa wazee, ambapo mpaka sasa kuna jumla ya madirisha 2,335 mahususi kwa ajili ya kutolea huduma za matibabu kwa wazee.
Vilevile, katika kuimarisha uratibu serikali imeanzisha utaratibu wa kuwa na timu za uratibu katika vituo vya kutolea huduma za afya ambazo zinajumuisha Daktari, Afisa Ustawi wa Jamii na Muuguzi.
Aidha amesema kuwa Serikali inatambua umuhimu wa Wananchi kujiandaa kabla ya kuzeeka kuwa ni suala la kuzingatiwa wakati wote wakiwa katika shughuli za kuzalisha mali na kujipatia kipato.
Jambo hili litawawezesha Wananchi kukidhi mahitaji yao ya msingi na kujiwekea akiba ya baadae kwa ajili ya maisha ya uzeeni.
Pia amewambusha kuwa sote tuendelee kutimiza wajibu wetu kuwalinda wazee dhidi ya vitendo viovu vinavyohatarisha maisha na uhai wao. Kwa kufanya hivyo tutaendelea kuenzi na kuthamini ujuzi, uzoefu na michango ya wazee katika maendeleo ya Taifa letu. Ni ukweli ulio wazi kuwa Wazee ni Hazina kubwa na Tunu ya Taifa letu, tuwapende, tuwaheshimu na kuwalinda.
Kwa upande wake Katibu Mkuu WIzara ya Afya-Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii, Dk. John Jingu ameiasa jamii kuwatunza wazee katika jamii zao na kutowatekeleza na kuwaacha peke yao bali wawanagalie na kuwatunza kama wao walivyotunzwa wakiwa watoto.
Ameongeza kuwa Wazee pia wanapatwa na Ukatili wa kiuchumi kwa kunyang’anywa mali zake na watoto na hata ndugu zake hivyo kuitaka jamii kuoaza sauti kupinga ukatili wowote unaofanywa dhidi ya wazee.
Upande wake Meneja Programu wa Shirika la Wazee la HelpAge Tanzania Joseph Mbasha amesema kuwa Shiirka hilo limashirikiana na Serikali kutekeleza afua mbalimbali zinazosaidia kuwalinda wazee kuondokana na vitendo vya ukatili dhidi ya wazee katika maeneo mbalimbali nchini.
Naye Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu, Dk. Fatma Khalfan ameipongeza Serikali kwa kuwalinda wazee kwa kutekelza afua mablia na kutoa wito kwa jamii kuachana na vitendo vya uakatili dhidi ya wazee kwa vinaenda kinyume na haki za binadamu.
KIla Juni 15 ya mwaka dunia inaadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee yenye lengo la kuangalia changamiti zinzazowakabili wazee na kuzitafutia utatuzi kwa mstakabali wa ustawi wa wazee na kwa mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu isemayo “Tupaze Sauti Kupinga Ukatili Dhidi ya Wazee,” amesema.