26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mapya yaibuka Kenya waliozuia mahinda ya Tanzania

Nairobi, Kenya

Waziri wa Kilimo Peter Munya ameipokonya mamlaka Taasisi inayohusika na kutoa idhini ya kuingiza nafaka nchini Kenya katika maeneo ya mpaka. (AFA)

Waziri Munya amesema serikali itaitumia taasisi ya ukaguzi wa usalama wa mazao (Kephis) kuhakikisha kuwa mahindi yana viwango vinavyohitajika.

“Kuanzia sasa, AFA haitasajili mahindi ambayo tayari yamesajiliwa na Kephis. Sisi sote tunahimiza kuchukuliwa sampuli moja wakati malori ya kampuni moja yanapoingiza bidhaa,’’ amesema Bw Munya Ijumaa iliyopita wakati alipotembelea mpaka wa Namanga.

Hatua hiyo imekuja baada ya agizo la wiki iliyopita la Rais Uhuru Kenyatta kwa Waziri Munya kuhakikisha idhini ya kuingiza mahindi inapatikana haraka wakati wa ziara yake ya kiserikali ya siku mbili na rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu hassan.

Awali Kenya ilipiga marufuku mara moja ununuzi wa mahindi kutoka mataifa jirani ya Tanzania na Uganda.

Kulingana na barua iliyoandikwa na Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya kilimo na chakula, Kello Harsama kwa Pamela Ahago ambaye ni Kamishna wa forodha katika mamlaka ya ushuru nchini Kenya KRA, ununuzi huo ulisitishwa baada ya uchunguzi kubaini kwamba mahindi kutoka mataifa hayo mawili sio salama kwa matumizi ya chakula cha binadamu.

Mamlaka hiyo imekuwa ikifanya uchunguzi kuhusu usalama wa chakula kinachoingizwa nchini Kenya .

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles