Na Jeremia Ernest, Dar es Salaam
Kampuni ya Seams Apparel Limited pamoja na wadau wa mitindo Ety’screation wameandaa harambe ya kuchangia watu wenye mahitaji maalum katika jamii.
Harambee hiyo itafanyika Mei 8, mwaka huu Osterbay jijini Dar es Salaam, kwa kushiriki katika Iftari ambayo itafwatiwa na onesho la mavazi kutoka kwa wabunifu wa Sems Appael Limited.
Akizungumza na www.mtanzania.co.tz Mratibu ya shughuli hiyo, Sammy Diwani ‘Etyscreations,’ amesema wameadhimia kukusanya fedha ambazo zitakabidhiwa kwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshuhulikia Watu wenya Ulemavu, Ummy Nderiananga, kwa ajili ya kununua vifaa vya watu wenyewe ulemavu.
“Tutakuwa na Ifutari ya pamoja, baada ya hapo kutafanyika onyesho la mavazi ambayo yatanadiwa na kuuzwa kwa ajili ya kupata fedha za kusaidia watu wasio jiweza.
“Pia katika shuhuli hiyo itahudhuriwa na mgeni rasmi kutoka katika ofisi ya Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshuhulikia Wenya Ulemavu ambaye atamuwakilisha Naibu Waziri Ummy,” amesema Etyscreation.
Aliongeza kuwa wana karibisha watu wote kushiriki katika changizo hilo kwa kununua kadi shilingi 50000 kupitia mtandao wa Nilipe app.