27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yaombwa kutupia jicho sheria za usajili wa VICOBA

Na Upendo Mosha,Rombo

Wanawake wanaojihusisha na Taasisi ndogo za kifedha (VICOBA) hususani wajasiriamali wadogo, wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro wameiomba Serikali kuangalia upya sheria ya usajili wa taasisi hizo kwa madai kuwa ni kandamizi.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mrere, Kata ya Kataranga Mrere, wilayani humo, ulioandaliwa na diwani wa kata hiyo, Venance Maleli, wananchi hao wamesema pamoja na kuwepo kwa baadhi ya vipengele venye manufaa kwao pia ni kandamizi.

Adela Priscus amesema pamoja na kwamba sheria hiyo imelenga kuimarisha taasisi ndogo za kifedha bado inamapungufu makubwa na kwamba ni vema serikali ikaipitia upya kwani ni kandamizi.

“Hii sheria imekuja wakati hatujajiandaa vizuri na kwa namna tulivyoiona imekaa kikandamizi sisi ni wajasiriamali wadogo wanatuletea sheria hii wakati hatujajiandaa kuipokea na kama vile inatutega sisi,”alisema

Fina Moshi,mjasiriamali wa ndizi,alisema hawana imani na sheria hiyo iliyo pitishwa na BOT na kwamba fedha wanazo zipata wanazipata kwa tabu kubwaa na ni wakati sasa wa serikali kuangalia upya namna ya kuiondoa sheria hiyo kwani inakandamiza wananchi wanyonge.

“Kabla ya Sheria mpya ya kutaka kusajili upya vikundi vyetu tulisha visajili na vinatambulika sasa sheria hii hatuelewi inalenga nini hatujapewa uelewa wa kutosha….watuelemishe faida yake kwanza,”alisema

Akizungumza kuhusu usajili huo, Ofisa Maendeleo Msaidizi wa wilaya hiyo,Edwin Wilson,alisema vikundi hivyo vinasajiliwa bure na kwamba serikali haina lengo la kuwatoza kodi badili ni kwaajili ya kuweka kumbukumbu sawa.

“Lazima sheria ifuatwe jambo hili halina lengo la kuwakandamiza kama mnavyofikiri na pia vijana na watu wenye ulemavu mjisajili kwenye vikundi muweze kupata mikopo inayo tolewa na Halmashauri ambayo ni asilimia kumi ya mapato yatokanayo na makusanyo ya ndani,”alisema

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles