Na Mwandishi Wetu, Mbulu
Benki ya NMB imeshatoa zawadi zenye thamni ya zaidi ya Sh milioni 60 kuzawadia washindi wa promosheni ya Bonge la Mpango inayohamasisha utamaduni wa watanzania kujiwekea akiba benki.
Hayo yalibainishwa jana na Meneja wa Benki ya Nmb, Kanda ya Kati ,Nsolo Mlozi wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi ya pikipiki ya miguu mitatu kwa mshindi, Paulina Mushi makazi wa wilayani Mbulu.
Nsolo alisema mpaka sasa benki hiyo imeshakabidhi zawadi za kampeni ya bonge la mapango zenye thamani ya zaidi ya sh milioni 60 kwa washindi wa maeneo mbalimbali hapa nchini.
“Mpaka sasa tayari kupitia kampeni yetu hii ya bonge la mpango tumeshatoa zawadi za fedha tasilimu na vitu mbalimbali vyenye tahamani ya sh milioni 59 ambazo zimeenda kwa wateja wetu wa maeneo mbalimbali hapa nchini ,”alisema
Alibanisha kuwa kwenye kampeni hiyo benki ya NMB ilikabidhi zawadi mabalimbali zikiwemo fedha tasilimu pamoja na pikipiki za magurudumu matatu za kubeba mzigo maarufu kwa maguta.
Meneja Uhusiano wa amana za wateja kutoka NMB Makao makuu ,Monica Job, alisema wateja walioshinda katika kampeni hiyo wanatoka katika mikoa ya Dar es Salaam,Mbeya,Tanga,Mwanza ,Manyara,Tabora,Morogoro na Pwani.
Bwana Nsolo alieleza kwamba bahati nasibu ya benki hiyo, ilianza mwezi wa pili mwanzoni inalenga kujenga tabia ya wananchi kujiwekea akiba pamoja na kurudisha kiasi cha fedha kwa wananchi.
Alizitaja baadhi ya zawadi zinazoshindaniwa kuwa ni fedha taslimu,kwa watu kumi kila wiki wanajishindia hadi Sh 500,000, pikipiki ya miguu mitatu mbili kila wiki,gari dogo la kubeba mizigo aina ya Kilikuu kila mwezi na gari la kifahari aina ya Toyota Fortuner ambavyo vyote hadi bahati nasibu hiyo inamalizika zitatumia zaidi ya Sh milioni 550.
Kwa upande wake Mshindi wa pikipiki ya magurudumu matatu – Paulina Moshi aliishukuru NMB kwa zawadi hiyo iliyompatia.
“Mimi hapa ni mjane mume wangu amefariki leo anatimizi siku 55 tangu kifo chake, naona Mungu kupitia NMB ameona unyonge wangu na kunipatia zawadi hii itakayosaidia kuingiza kipato cha familia yangu ,Mungu awabariki sana benki hii”alisema .
Alisema anakumbuka ilikuwa machi 17 mwaka huu alipigiwa simu na Mtu kutoka Nmb akimjulisha ameshinda zawadi kupitia bonge la mapango lakini hakuamini mpaka alipofika kwenye tawi la NMB Mbulu kuhakikishiwa kuwa ni kweli.
Pia alisema yeye hakujua kuhusu kampeni hiyo lakini alikuwa na utaratibu wa kuweka fedha kwenye akaunti yake hivyo ushindi huo hauna upendeleo na wengine waendelee kuweka fedha kwenye akaunti zao na kufungua akauti mpya watajishindia zawadi hizo.
Aliongeza kuwa hakutegemea kuona upendo alioonyeshwa na wafanyakazi wa NMB kwa kuwajali mpaka pikipiki hiyo kufikishwa nyumbani kwake eneo la mtaa wa Ujenzi,Halmashauri ya Mbulu.