23 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

ATCL kuanza safari za Guanzou, China

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Hatimae Safari za ndege za ATCL kutoka Tanzania kuelekea Guanzou, China zinatarajiwa kuanza Mei 08,2021 mara moja kila baada ya wiki mbili licha ya kuendelea kuwepo janga la corona.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula ameyasema hayo wakati wa mazungumzo yake na Balozi wa China hapa nchini, Wang Ken na kuongeza kuwa safari hizo zitaongeza kwa kuzingatia muenendo wa maradhi ya COVID 19.

Kwa upande wake Balozi wa China hapa nchini, Wang Ke amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa hatua yake ya kukutana na Jumuiya ya wafanyabiashara kutoka China na kuongeza kuwa hatua ya uwepo wa safari za ndege za moja kwa moja kutoka Tanzania hadi China ni fursa ya kukuza biashara na uwekezaji na kwamba China itaendelea kuunga mkono dhana ya diplomasia ya Uchumi isiyoingilia masuala ya ndani ya kwa faida ya pande zote mbili.

Pia Balozi Mulamula kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi kutoka Ujerumani,Ubelgiji na Israel ambapo masuala makubwa yaliyojadiliwa ni pamoja na mashirikiano yatakayokuza uchumi na biashara lakini pia miradi mbalimbali itakayochochea ustawi wa jamii ikiwa ni pamoja na elimu,afya na miundombinu.

Balozi anayeiwakilisha Israel hapa nchini, Oded Joseph amesema Israel itaendelea kushirikiana na Tanzania katika masuala mbalimbali hususani katika kukuza ujuzi wa kilimo chenye tija kwa vijana ambapo kwa sasa Israel inawapokea vijana kutoka Tanzania waliohitimu katika vyuo vya kilimo kwa lengo la kujifunza kwa vitendo nchini humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles