New York, Marekani
Mtayarishaji nyota wa muziki nchini Marekani, Rudy Henry, ametamba kwamba lebo yake ya Russian Movements Records, imekuwa ikipata mafanikio tangu alipoianzisha mwaka 2015.
Rudy Henry ambaye amebobea kutengeneza muziki aina ya Dancehall, Reggae na Soca Caribbean, amesema siri ya mafanikio yake ni kuwa mbunifu na kuwa na ‘sound’ mpya kila siku jambo linaloendelea kumpa heshima yeye na bidhaa zake za nguo chapa Russian Mvmts Wear.
Prodyuza huyo ameongeza kuwa miongoni mwa wasanii aliofanya nao kazi kwa mafanikio makubwa ni Linky First, Black Ryno, Cooyah, Ambi, Mlingo &Matta, G Don Subance na hivi karibuni ameachia wimbo Nuh Medz wa msanii Flexxx.
“Iko wazi katika soko la Dancehall, Reggae na Soca Caribbean hapa Marekani nimejitahidi kufanya biashara nzuri hasa ninapokutana na wasanii wenye uwezo wa tunatengeneza ‘hit’ tangu 2015 nilipounda Russian Movements Entertainment na tukaachia mradi wa msanii Linky First unaoitwa Rock andCome In,” amesema.