Upendo Mosha,Babati
SERIKALIimeagiza wataalamu wa Kilimo kutoka Katika taasisi mbalimbali za utafiti kuwekeza na kutafiti aina bora za mbolea na kutoa utaalamu huo kwa kiwanda Cha mbole Cha Minjingu hatua ambayo itasaidia nchi kuacha kuagiza bidhaa hizo nje.
Agizo hilo lilitolewa na waziri wa Kilimo, Prof Adolf Mkenda wakati wa ziara ya kutembelea kiwanda hicho akiongozana na wataamu kutoka Katika taasisi hizo,wilayani Babati,Mkoani Manyara.
Mkenda alisema niwajibu wa watalamu wa utafiti wa kilimo Katika mazao mbalimba kufanya utafiti utakaosaidia kugundulika kwa mbole Bora na zenye matokeo mazuri kwa wakulima Jambo ambalo litapunguza gharama za uagizwaji wa mbole kutoka nje ya nchi.
“nawaagiza wataalumu kutoka Katika taasisi za Kilimo kufanya utafiti utakaosaidia kiwanda hicho Cha Minjingu kuzalisha mbolea zile ambazo zinafanya vizuri ambazo tumekuwa tukiagiza Nje ya nchi…njia ya kuzalisha mnazo na sio Siri”alisema Mkenda
Alisema serikali imekuwa ikitumia zaidi ya Dola milioni 200 kuagiza tani laki Saba za mbole kwa mwaka kutoka nje kwa kutumia fedha za wakulima na kwamba iwapo bidhaa hiyo itazalisha nchini italeta tija zaidi kwa taifa tofauti na ilivyo sasa.
“kimsingi tunatumia pesa za wakulima ni hasara …kile ambazo kinaweza kuzalishwa hapa ambapo hakiwezi kutuongezea bei kizalishwe hapa mambo ya pembejeo tukiendelea kuagiza hatutasonga mbele”alisema
“watafiti wasaidieni Hawa wazalishaji wetu wa ndani kutengeneza bidhaa zenye ubora na mnafahamu Minjingu wanaweza kufanya tumsaidie afanye hivyo maana kwanza watu wetu watapata ajira TRA watakuwanya mapato zaidi na Taifa kupata mapato mengi zaidi”alisema
Naye Mkurugenzi wa Kiwanda Cha Minjingu,Tosky Hans,alisema kiwanda hicho kimejiwekea mkakati wa kuongeza uzalishaji kutoka Tani laki Moja Hadi kufikia Tani laki Tano ifikapo Mwaka 2025 lengo likiwa ni kukithi nahitaji ya soko la ndani.
“Tunafahamu serikali imeweka malengo la kukuza sekta ya Kilimo tumeanza kuzungumzia na taasisi za kifedha kwaajili ya kutukopesha na. Kupanua kiwanda chetu, kiwanda kinatengeza mbolea za ainatofauti tofauti kulingana na mazao na mbolea hizi zimesheni Aina mbalimbali za virutubisho vya udongo
Aidha alisema kiwanda hicho kinakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo Ile ya serikali kutolipa malimbikizo ya Deni la mbole za ruzuku la Mwaka 2015/2016 na kulipishwa Kodi za VAT kuingiza malighafi.
Mkuu wa mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti,alisema baadhi ya watafiti wa Kilimo wamekuwa Ni changamoto kutokana na kuacha kufanyakazi na wakulima na kubaki maofisini Jambo ambalo wanapaswa kubadilika kwa lengo la kuketa maendeleo Katika sekta ya Kilimo