24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Waitara aitaka TRC kutoa huduma bora

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Serikali imelitaka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhakikisha linatoahuduma bora na za viwango kwa Watanzania mara baada ya mradi waujenzi wa reli ya kisasa ya (SGR) sehemu ya Dar es Salaam hadi Morogorokukamilika na kuanza kutoa huduma ifikapo mwishoni mwa mwezi Agosti, mwaka huu.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, kuhusu hatua ya ujenzi wa Jengo la abiria katika stesheni ya Dar es Salaam Morogoro wakati Naibu Waziri huyo alipokagua maendeleo ya ujenzi wa reli stesheni, mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salam

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara, kufuatia wasiwasi wa wananchi kuhusu masuala yamiundombinu ya umeme wa reli hiyo ambapo pamoja na mambo mengine Naibu Waziri huyo amesema kuwa Serikali kupitia Shirika hilo imejidhatitikwa kuweka vyanzo vya umeme vitatu tofuati na vichwa vya kutumiadizeli ili kutatua changamoto zozote zitakazojitokeza.

“Napenda kuwatoa wasiwasi Watanzania kuwa Serikali kupitia TRCimejipanga sawasawa kuhakikisha umeme hautakuwa changamoto wakatiwa uendeshaji wa treni hii,” amesema Waitara.

Aidha, Waitara amelitaka Shirika hilo kujipanga na kuhakikisha kuwawataalam wazawa waliopata ujuzi kwenye mradi huo wanatumikaipasavyo mara baada ya mradi kukamilika.

Waitara, amelipongeza Shirika hilo kwa kuajiri watalaam na kusimamiavizuri mradi huo kwa sehemu ya Makutupora hadi Morogoro na Morogorohadi Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara (kulia), akitoa malekezo kwa Mhandisi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) Morogoro, Blasius Mwita, wakati alipokagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha Stesheni ya Morogoro, mwishoni mwa wiki, Mkoani Morogoro. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa.

Naibu Waziri Waitara amemhakikishia Mkurugenzi wa TRC kuwa Serikaliitaendelea kuhakikisha inatoa fedha ili mradi uweze kukamilika na Watanzania wafaidi matunda ya Serikali yao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Masanja Kadogosa,amesema kuwa TRC imeshaajiri wahandisi zaidi ya 200 ambao kwa sasa wamewekwa kwenye miradi ili kupata ujuzi na uendeshaji wa reli hiyo yakisasa mradi utakapokamilika.

Kuhusu upatikanaji wa mabehewa Kadogosa amefafanua kuwa tayari manunuzi yako kwenye hatua nzuri na vichwa vitawasili mapema Julai, mwaka huu na majaribio ya treni ya kwanza kwa sehemu ya Dar es Salaam hadi Morogoro yatafanyika Agosti, mwaka huu.

Naye, Meneja Mradi wa sehemu ya Morogoro – Dar es Salaam, Mhandisi Simon Mmbaga, amesema mradi huo kwa sehemu ya Dar es Salaam hadi Morogoro umeshakamilika na asilimia zaidi ya 93 na kazi zinazoendelea kukamilishwa ni pamoja na kuunganisha mifumo mbalimbali katika vituo.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara amekamilisha ziarayake ya siku mbili ambapo amekagua maendeleo ya ujenzi wa reli yaKisasa ya SGR kwa sehemu ya Makutupora hadi Morogoro na Morogoro hadi Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles