Mogadishu
Shirika la kimataifa la misaada ya kibinaadamu limesema katika msimu huu mamilioni ya watu nchini Somalia hawatakuwa na chakula cha kutosha kufuatiwa na wimbi kubwa la nzige, hali mbaya ya hewa na kiwango cha chini cha mvua.
Shirika la Save the Children limesema, mimea na mazao ya mboga mboga yanatarajiwa kupungua kwa 80% na mpato yatokanayo na mauzo ya mifugo, ambayo ni uti wa mgongo wa uchumi wa Somalia, yanatarajiwa kushuka hadi 55%.
Shirika hilo limesema kuwa mwaka huu familia za hali ya chini zinakadiriwa kupata asilimia 15% ya chakula kutokana na mazao, huku baadhi ya Watoto nchini humo tayari wanaugua ugonjwa wa utapiamlo kwa kupata mlo mmoja kwa siku.
Wasomali wanakabiliwa na changamoto ya ghasia za muda mrefu za magaidi wa kiislamu, hali mbaya ya kisiasa na kutokuwa na serikali kuu henye ufanisi kwa muda wa miaka 30.