Juba, Sudan Kusini
Katibu wa habari wa Gavana nchini Sudani kusini, Alinadro Lotok ametoa ripoti ya shambulio la kigaidi lililotokea jimbo la Equatoria mashariki mwa nchi hiyo.
Shambulio hilo lililofanya na kikundi cha watu wa jamii ya Buya na kusababisha vifo vya watu 20 huku Gavana Louis Lojore wa nchi hiyo akinusurika kupoteza Maisha.
Lotok alisema Gavana Lobong alikuwa katika kambi ya kijeshi Camp 15 kutuliza hali ya taharuki katika eneo hilo baada ya shambulio la siku ya Jumapili dhidi ya kituo hicho na kusababisha vifo vya watu 17.
Hata hivyo baada ya mashambulizi ya risasi ya muda wa masaa mawili kitengo cha ulinzi wa gavana na askari wa kambi ya jeshi ya Camp 15 walifanikiwa kudhibiti jamii hiyo ya watu wa Buya.
Miongoni mwa waliofariki katika shambulio hilo ni walinzi wa gavana na mke wa askari huku watu watatu wakijeruhiwa.