Na Jeremia Ernest, Dar es Salaam
Usahili wa kusaka wanamitindo watakao pamba tamasha la Lady in Redy Februari 13, umefanyaika Masaki Element jijini Dar es Salaam.
Usahili huo uliofanyika juzi Jumamosi uliendeshwa na majaji wa tano ambao ni wabunifu nguli hapa nchini, Asia Idarus, Mustapha Hassanali, Ally Remtula, Martin Kadinda na Jamila Veraswai.
Tamasha la Lady in Red, linafanyika kila mwaka mwezi wa pili kipindi cha sikuku ya napenda nao kwa ajili ya kuinua vipaji vya wabunifu kwa kuonyesha kazi zao mwaka huu inaratibiwa na kampuni ya Hugo Domingo pamaja na Chama cha Wabunifu nchini.
Akizungumza na wandishi wa habari mwasisi wa onyesho hilo, Asia Idarus Hamsini, ‘Mama wa Mitindo,’ amesema mwaka tamasha hilo litafanyika katika ubora wa juu kuliko miaka iliyopita.
“Tokea ni stafu kuandaa tamasha la Ledy in red limeshuka kiwango chake lakini mwaka huu tumepata waendeshaji ambao wana kiu ya kuinua tasnia yetu hivyo litakuwa ni tamasha lenye hadhi ya kimataifa,” anasema mama wa Mitindo.
Ameongeza kuwa mpaka sasa wabuni takribani 35, wamesha jisajili kuonyesha kazi zao siku hiyo kupitia wanamitindo 30 ambao wamepatikana leo katika usahili tamasha litafanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.