29.2 C
Dar es Salaam
Monday, December 16, 2024

Contact us: [email protected]

Watumishi TBS, WMA watakiwa kufanyakazi kwa uadilifu

Na Ramadhan Hassan, Dar es Salaam

Waziri wa Viwanda na Biashara, Geoffrey Mwambe amewataka watumishi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Wakala wa Vipimo (WMA) kufanya kazi kwa uadilifu, weledi  na kuwafikiria wafanya biashara wakati wakitoa huduma kwa wafanyabiashara ili kuendelea kutengeneza taswira nzuri ya bidhaa  za Tanzania katika soko la ndani nan je ya nchi.

Waziri Mwambe aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na Menejimenti na wafanyakazi wa TBS na WMA alipofanya ziara katika taasisi hizo akiambatana na Naibu Waziri wa Viwanda, Exaud Kigahe pamoja na baadhi ya wakurugenzi wa Wizara ya Viwanda na Biashara.

Waziri Mwambe ameiagiza TBS kufanya ukaguzi wa bidhaa kwa kushirikiana na taasisi nyingine zinazohusika na ukaguzi wa mizigo bandarini na mipakani ili kupunguza muda unatumika kugagua bidhaa hizo,kupunguza mianya ya rushwa na kurahisisha utoaji wa mizigo hiyo kwa haraka.

Aidha, ameitaka TBS kupunguza muda wa kuandaa viwango kutoka miezi 9 hadi miezi 3 na muda wa usajili wa bidhaa na kutoa alama ya ubora kutoka miezi 3 hadi mwezi mmoja ili kuwarahisishia wajasiliamali kuwezakufanya na kukuguza biashara zao kwa urahisi.

“Niwahimize TBS mfanye kazi kwa karibu  na Maafisa Biashara wa Halmashauri ili kurahisisha utoaji wa elimu na usimamizi wa viwango kwa wajasiriamali  ili kupanua uwigo wa utoaji huduma na kuwafikia wajasiriamali wengi walioko katika halmashauri hizo.

“Vilevile niwalelekeze TBS kufanya kazi kwa pamoja na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO)  na  Balaza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) katika kuandaa Viwango na miongozo yenye vigezo rahisi vitakavyowawezesha wajasiriamali wetu kuanzisha viwanda vidogo  majumbani ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa, kukuza biashara kuongeza ajira nakuongeza pato la taifa,” amesema Mwambe.

Naye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amezitaka TBS na WMA kuhakikisha zinasimamia viwango na ubora pamoja na vipimo sahihi vya bidhaa za Tanzania ili kuziwezesha bidhaa hizo kuingia katika soko la ushindani ndani na nje ya nchi kwa ufanisi.

Aidha ameziagiza taasisi hizo kuendelea kuimarisha ukaguzi wa bidhaa zinazotoka nje ya nchi zinakuwa na viwango navipimo sahihi ili kuiepusha Tanzania kuwa dampo la bidhaa hafifu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles