24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TAKUKURU Tabora waokoa zaidi ya Sh milioni 300

Na Allan Vicent, Tabora

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Tabora wamefanikiwa kuokoa Sh milioni 330 za wananchi, Taasisi za umma na Vyama vya ushirika vya msingi katika kipindi cha miezi mitatu.

Hayo yamebainishwa jana na Kaimu Mkuu wa Taasisi hiyo mkoani hapa, Mashauri Elisante alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari.

Alisema kuwa fedha hizo zimeokolewa kati ya mwezi Oktoba na Desemba mwaka jana kutokana na uchunguzi na ufuatiliaji wa kina wa malalamiko yaliyowasilishwa na wananchi katika taasisi hiyo.

Alifafanua kuwa Sh mil 48.7 ziliokolewa kutoka katika vyama vya ushirika vya msingi (AMCOS) na SACCOS na kurejeshwa kwa wahusika baada ya uchunguzi kubaini uwepo wa ubadhirifu.

Aliongeza kuwa Sh mililioni 62.1 ziliokolewa kutoka kwa wadaiwa sugu wa mapato ya halmashauri baada ya kufuatiliwa na kuzilipa katika akaunti ya halmashauri husika huku kiasi cha sh mil 14.7 zikirejeshwa kwa taasisi nyingine.

Aidha alibainisha kuwa kiasi cha Sh milioni 195.8 ambazo wakulima wa tumbaku walikuwa wakidai makampuni wanunuzi ziliokolewa na kulipwa wahusika kupitia vyama vyao vya msingi (AMCOS).

Elisante alitaja fedha nyingine zilizookolewa na kulipwa wahusika kuwa ni Sh milioni 5.5 za mikopo kutoka kwa wakopeshaji wasio kwenye mfumo rasmi wa taasisi za kifedha na malipo ya Sh milioni 10.2 za watumishi wa muda waliokuwa wamedhulumiwa mishahara yao.

Alieleza kuwa katika kuhakikisha vitendo vya rushwa vinaendelea kudhibitiwa na kukomeshwa Mkoani humo wamefanya mikutano ya kuelimisha makundi mbalimbali ya kijamii ikiwemo kufungua klabu za wapinga rushwa katika shule za sekondari na vyuo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles