25 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 17, 2024

Contact us: [email protected]

TACAIDS yaombwa kutoa elimu kwa makundi maalum

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) imeombwa kutoa elimu sahihi ya kujikinga na maanbukizi ya mapya ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa makundi maalum ikiwa ni pamoja na kutumia wakalimani wa lugha.

Washiriki wa semina hiyo wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya mafunzo hayo kufunguliwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ACAIDS, Jumanne Issango.

Wito huo umetolewa leo Januari 11, jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Chama Cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) Mkoa wa Dar es Salaam, Habibu Mrope kwenye semina ya siku mbili ya kuwajengea uwezo wawakilishi wa watu wenye ulemavu wa kusikia (Viziwi) Mkoa wa Dar es Salaam.

“Ni kweli kwamba tume ya kudhibiti ukimwi imekuwa ikifanyakazi nzuri ya kuelimisha umma kwenye mambo mbalimbali yakiwamo ya maambuzi lakini bado kuna changamoto kwa makundi maalumu katika kufikiwa na elimu hii.

“Mfano ukiangalia kwenye matangazo mbalimbali ambayo mmekuwa mkiyatoa kwenye vyombo vya habari bado ni changamoto kwetu kuweza kuelewa kwamba yanazungumzia nini kutokana na kutokuwa na mkalimani wa lugha.

“Hivyo ni muhimu jambo hilo likapewa mkazo kwani kama tunavyofahamu kwamba sisi ndio tulioko kwenye hatari kubwa ya maambuzi na ndiyo maana utakuta tukiambukizwa kwani ni rahisi kulaghaiwa,” amesema Mrope.

Mrope amesisitiza umuhimu wa taarifa sahihi za VVU kuwafikia kundi maalum la walemavu kupitia matangazo mbalimbali yanayorushwa katika vyombo mbaloimbali vya habari kuzingatia lugha za alama, kwamba yatachangia kwa kiasi kikubwa elimu kufika kwa makundi hayo kwa haraka.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Jumanne Issango, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Dk. Loenard Maboko, amesema wamepokea changamoto hiyo na kwamba watazifanyia kazi katika kuhakikisha kuwa elimu inayafikia makundi hayo yote.

“Huu ni mwendelezo wa Tacaids katika kuhakikisha kwamba tunayafikia makundi yote maalum nchini lengo likiwa ni kupunguza kabisa maambukizi mapya ya ukimwi.

“Tunajua changamoto mnayoipata ikiwamo kufikiwa na elimu ambapo hata matangazo tunayoyatoa yamekuwa siyo rafiki kwenu ikiwamo yale ya Redio na Televisheni kutokana na kutokuwa na Wakalimani, lakini niwaahidi kuwa kupitia idara husika tutajitadi kuhakikisha kwamba tunalifanyia kazi hilo na kutoa kipaumbele kwa makundi maalumu likiwemo la viziwi ili kufikia Tanzania isiyo na unyanyapaa pamoja na maambukizi ya ukimwi kama ambavyo tunasema kwamba hakuna mtu kuachwa  nyuma,” amesema Isango na kuongeza kuwa:

“Niseme tu kwamba serikali tumejipanga kuweza kuzifanyia kazi changamoto hizi ikiwamo kuongeza mafunzo ya watu wanaofanyakazi ya ukalimani ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya wahusika kwani mbali na masuala ya Ukimwi pia wanatakiwa kutumika kwenye nyanja mbalimbali.

“Kwani kuna watu ambao hawaoni, hawasikii na aina nyingine za ulemavu hivyo lazima tutoe elimu,” amesema Issango.

Aidha, ametoa wito kwa wadau wengine wote kuhakikisha kuwa suala la kuwashirikisha wakalimani linapewa kipaumbele kwa manufaa ya watu wenye ulemavu.

“Pia kwenye utoaji wa takwimu watu wenye ulemavu watajwe kwa namna yao ya pekee na siyo tutoa tu kiujumla,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles