30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Rais Trump, mkewe watembelea askari Irak

BAGHDAD, IRAK

RAIS wa Marekani Donald Trump na mke wake Melania Trump wamefanya ziara ya kushtukiza kwa kuwatembelea wanajeshi wa Marekani nchini Irak.

Wakiwa pamoja na mshauri wa usalama wa taifa John Bolton walitumia ndege ya Air Force One kwenda kambi ya jeshi ya  al-Asad, magharibi mwa mji mkuu Baghdad kukutana na wanajeshi hao.

Walisafiri kwenda huko usiku wa siku ya Krismasi kuwashukuru kwa huduma yao, mafanikio na kujitolea kwao, Ikulu ya Marekani, White house imesema.

Ziara hiyo inafanyika siku chache baada ya Waziri wa Ulinzi, Jim Mattis kujiuzulu kutokana na kutoelewana kuhusu sera za Trump eneo hilo.

Marekani ina wanajeshi 5,000 nchini Irak kuunga mkono serikali katika vita dhidi ya kundi lijiitalo Dola la Kiislamu (IS).

Hata hivyo, mkutano uliopangwa kati ya Trump na Waziri Mkuu wa Irak, Adel Abdul Mahdi ulifutwa.

Ofisi ya Mahdi ilisema hiyo ni kwa sababu ya kutokubaliana jinsi ya kuendesha mkutano huo.

Mazungumzo kwa njia ya simu kati ya viongozi hao badala yake yalifanyika na White House inasema Mahdi alikubali mwaliko wa kuzuru Marekani.

Katika ziara yake hiyo ya kwanza ya aina hiyo eneo hilo, Trump alipata makaribisho mazuri kutoka kwa wanajeshi wakati aliingia ukumbini na kutembea akiwasalimia wanajeshi na kupiga nao picha. Alisema sababu ya ziara hiyo ni kuwashukuru mwenyewe wanajeshi kwa kusaidia kuwashinda IS

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles