25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha Simba aeleza alivyojitabiria kichapo

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, amefichua kuwa alitarajia kikosi chake kupoteza mchezo wake  dhidi ya Mashujaa kutokana na wachezaji kutoonyesha dhamira ya dhati ya kupambana ili kupata ushindi.

Simba juzi ilitupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho (ASFC), baada ya kuchapwa mabao 3-2 na Mashujaa katika mchezo uliochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kipigo hicho kilikuwa mwendelezo wa kikosi cha Simba kutimuliwa katika mashindano hayo na timu zinazomilikiwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Katika mashindano yaliyopita, Simba  ilitupwa nje katika hatua kama hiyo na timu ya Daraja la Pili ya Green Warriors, baada ya kupoteza penalti 4-3 kutokana na dakika 90 kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Akizungumza baada ya mchezo dhidi ya Mashujaa yenye makao makuu yake mkoani Kigoma, Aussems aliwasifu wapinzani wao hao kwa kusema walicheza kwa umoja na mshikamano ili kupata ushindi.

“Wakati wa mapumziko niliwaambia wachezaji wangu, endapo wataendelea kucheza bila malengo hawataweza kupata ushindi, wapinzani wetu walikuwa wanacheza kwa moyo wote na walijitoa ili kuhakikisha wanapata ushindi kitu ambacho kimetokea,” alisema.

Aussems alizungumza sababu ya kuwatumia wachezaji wengi wa kikosi cha akiba katika mchezo huo kwa kusema kuwa alifanya hivyo ili kuwapumzisha wale waliocheza mechi ngumu ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nkana Red Devil ya nchini Zambia.

 Alisema walitoka kucheza mechi kubwa ambayo ilikuwa na presha na ndio maana aliamua kubadilisha kikosi kizima lakini hata hivyo, hawakuweza kuonyesha kiwango kizuri hali iliyowafanya wapoteze mchezo huo.

“Kwa bahati mbaya hawa niliowapa nafasi leo wameshindwa kufanya kazi sawa sawa.

“Walidhani kwamba itakuwa mechi rahisi lakini katika soka hutakiwi kumpuuza mpinzani wako, walitakiwa kuonyesha mabadiliko ili wapate matokeo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles