25 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 17, 2024

Contact us: [email protected]


MKUU wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo

mkoa wa Arusha una kata 20 zitakazoshiriki uchaguzi wa marudio baada ya waliokuwa madiwani wa Chadema kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

a mujibu wa taratibu za uchaguzi, mgombea anaposhindwa kurudisha fomu kwa msimamizi wa uchaguzi anakosa sifa ya mgombea.

Kwa mantiki hiyo, tayari wagombea wa kata saba wa CCM mkoani Arusha wamepita bila kupingwa.

agombea hao ni kutoka Kata za Ngoile, Ngorongoro, Pinyinyi na Soitsambu wilayani Ngorongoro. Alang’atadapash wilayani Longido, Lolkisale na Nararami wilayani Monduli.

Akizungumza na MTANZANIA jana mjini hapa, Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Arusha, Shabani Mdoe aliwapiga kijemba kuwa kushindwa kurejesha kwa makada wa Chadema kumesababishwa na ukata unaowakabili.

Alijigamba kuwa CCM kinaamini kitaongeza kata zaidi kwa kile alichodaiwa ni wagombea wa Chadema kuwa na upungufu mwingi ambao utawafanya washindwe kuendelea na ushindani.

“Hawa wagombea mbali na ukata wa fedha bado walishaona mbele kuwa wataangukia ‘pua’ na hivyo kuwavurugia malengo yao ya kisiasa mbeleni, hivyo waliona wasiweke historia mbovu ya kushindwa.

“Kwa ujumla tutashinda maeneo yote, kwani bado tunaweza kupata kata nyingine zaidi ya 12 ambazo tutapita bila kupingwa au kutokana kasoro mbalimbali za wagombea.

“Ninaamini kata ambazo tutashindana hazitazidi nane hivi,” alisema Mdoe.

Naye Katibu wa Chadema, Mkoa wa Arusha, Elisa Mungure alipopigiwa kwenye simu yake ya mkononi kuelezea changamoto iliyojitokeza kwa baadhi ya wagombea wao aliomba atafutwe muda mwingine.

“Naomba unipe muda, nitawapigia waaandishi wa habari bado nipo kwenye kikao kuna tatizo la wagombea wetu ku


chezewa rafu kila mahali,” alisema Mungure.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles