27.2 C
Dar es Salaam
Monday, September 26, 2022

JWTZ LATAKA MALALAMIKO RASMI TIBA MBOVU YA MTOTO


NA LUTENI  SELEMANI SEMUNYU

JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limemtaka mlalamikaji kuhusu tiba mbaya iliyotolewa kwa mtoto aliyevunjika mkono kuwasilisha malalamiko yake rasmi kwa uongozi wa Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo.

Akizungumza na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki, jijini Dar es Salaam, msemaji wa jeshi, Kanali Ramadhani Dogoli alimtaka mtu aliyejitambulisha kama mlalamikaji kuwasilisha malalamiko yake ili yafanyiwe kazi na ikibainika yana ukweli hatua zichukuliwe kwa wahusika.

“JWTZ linamtaka mlalamikaji alete taarifa kwa uongozi ili matukio haya kama yametokea tuchukue hatua kwa wahusika,” alisema Kanali Dogoli.

Alisema iwapo mlalamikaji atashindwa kufanya hivyo, jeshi litaaamini alikusudia kuichafua Hospitali ya Jeshi Lugalo kwa maslahi binafsi hivyo atachukuliwa hatua zinazostahili.

Kanali Kigoli alisema Julai 10, mwaka huu ilisambaa taarifa katika mitandao ya kijamii iliyokuwa na malalamiko kuwa kuna huduma zisizoridhisha katika kitengo cha mifupa cha Hospitali ya Jeshi Lugalo.

Kwamba taarifa hiyo ilieleza kuwa mtoto wa mlalamikaji ameungwa vibaya mkono na kutakiwa kupatiwa matibabu tena.

Alisema baada jeshi kupata taarifa, lilifanya uchunguzi kwa kupitiwa majina ya watoto wote waliotibiwa hosptalini hapo tangu Aprili hadi Juni 30, mwaka huu na kubaini hakuna mtoto aliyefika mara mbili kwa waliopata mivunjiko.

Naye Mkuu wa Tiba wa JWTZ, Meja Jenerali Dk. Denis Janga alisema amesikitishwa na taarifa hiyo na kwamba imewagusa wataalamu wa hospitali hiyo ambayo imekuwa ikitoa huduma kwa wananchi tofauti na majeshi mengine.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,044FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles