23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

20 Percent: Umri wangu ni mdogo kujihusisha na siasa

20%NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Abas Kinzasa ‘20 Percent’ amesema umri wake ni mdogo sana kujihusisha na masuala ya siasa kama ilivyo kwa rafiki yake, Afande Sele.
Akizungumza na MTANZANIA hivi karibuni, 20 Percent alisema kwa sasa anajipanga kurudi upya kwenye tasnia ya muziki, baada ya kuwa kimya kwa kipindi kirefu.
“Sijakaa kimya ili ni jihusishe na masuala ya siasa kama wengi wanavyofikiria, bali nina mipango yangu mingine kabisa,” alisema 20 Percent.
Alisema ukimya wake wa muda mrefu umekuwa na mipango mingi ya maendeleo nje ya sanaa, hivyo mashabiki wajiandae.
20 Percent ni miongoni mwa wasanii waliofanikiwa na kufanya vizuri katika tasnia ya muziki hapa nchini, ambapo kupitia nyimbo zake za Tamaa mbaya na Yanini malumbano alifanikiwa kujizolea tuzo tano katika tuzo za KTM mwaka 2010.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles