27.6 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Jela maisha kwa kumlawiti mtoto wa miaka 13

TWALAD SALUM -MWANZA

MKAZI wa Kijiji cha Old Misungwi wilayani Misungwi mkoani Mwanza, Saad Shabani (45), amehukumiwa na mahakama ya wilaya hiyo kwenda jela maisha kwa kosa la kulawiti mtoto  wa miaka 13 (jina limehifadhiwa).

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Eric Marley, alitoa hukumu hiyo jana baada ya kusikiliza shauri hilo ambapo upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi  saba.

Mahakama hiyo ilisikiliza pia mtoto aliyelawitiwa akieleza alivyofanyiwa na shahidi wa nne na tano ambao ni marafiki wa mtoto huyo ambao walieleza kwamba baada ya masomo rafiki yao aliwaambia wamsindikize kwa mtuhumiwa na kumuacha hapo ambapo kesho yake aliwaeleza kuwa alilawitiwa na kupewa Sh 700.

Mahakama pia ilikubaliana na ushahidi wa Dk. Mussa Mishamo, aliyemfanyia uchunguzi mtoto huyo na kukuta sehemu ya haja kubwa ilikuwa wazi kwa mm 12 na mishipa ya haja kubwa ilikuwa imefunguka na kidole cha kati kinaingia bila shida.

“Mahakama iliangalia kwenye kesi mbili za nyuma zilizotolewa maamuzi ya Athuman Ally Maumba na Babu Seya na wanae kwenye ushahidi wa utambuzi, hakuna shaka mtendewa alikuwa anamfahamu na alifika mara tano kwa mtuhumiwa na kufanyiwa vitendo hivyo,” alisema.

Marafiki zake walimtambua mtuhumiwa kuwa ni fundi baiskeli pia askari mpelelezi alikwenda kubaini chumba cha mtuhumiwa alimokuwa ameweka kitanda kilichosemwa na mtendewa,” alisema hakimu Marley.

Mtuhumiwa alipopewa nafasi ya kujitetea, aliomba kupunguziwa adhabu kwasababu ana mke na watoto watatu wanaosoma na dada yake anayeishi nae ni mgonjwa.

 Awali Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Ramsoney Saleh akisaidiwa na Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Juma Kiparo, alisema katika Kijiji cha Old Misungwi kwa mwaka 2017 tarehe tofauti, mshtakiwa anadaiwa kumlawiti mtoto huyo kwa mara tano na siku ya kwanza alimpa Sh 700.

Alisema mtoto huyo baada ya kuzoea kufanyiwa kitendo hicho, alikuwa anakwenda peke yake na mtuhumiwa kumpeleka kwenye chumba alichokuwa anatunzia vyombo vyake vya ufundi wa baiskeli katika soko la zamani la Misungwi na kumlawiti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles