BUCHAREST, ROMANIA
NCHI wanachama wa Umoja wa Ulaya wametangaza kuwa hawatamtambua kwa pamoja Juan Guaido kuwa rais wa mpito wa Venezuela, badala yake Nicolas Maduro atatambulika kama kiongozi wa serikali ya nchi hiyo.
Uamuzi huo ulifikiwa kwa pamoja katika mkutano ulioitishwa katika mji mkuu wa Romania, Bucharest, juzi ambako mawaziri wa mambo ya nchi za nje wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuunda tume ya mashauriano pamoja na mataifa ya Amerika Kusini.
Hadi wakati huu pekee bunge la Ulaya ndilo lililomtambua Juan Guaido kama rais wa mpito. EU wameafiki kuwa muda uliowekwa na Ujerumani, Ufaransa, Uingereza na Uhispania wa kumtaka Rais Nicolas Maduro aitishe uchaguzi.
Hata hivyo, muda uliotakiwa kuitishwa uchaguzi unamalizika mwishoni mwa wiki hii, ambako nchi hizo zilisema endapo atashindwa kuitisha uchaguzi huo, Umoja wa Ulaya umepanga kumuunga mkono Juan Guaido.