32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

ZSSF yatoa ufafanuzi kiinua mgongo kwa wastaafu

Na KHAMIS SHARIF

-PEMBA 

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), imeitaka jamii kisiwani Pemba kuelewa kwamba dhana ya mafao ya kiinua mgongo kwa mwanachama wa mfuko huo pale anapostaafu hayabakishwi kwa ajili ya kulipwa pensheni.

Hayo yalisemwa jana katika mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari na Ofisa Sheria wa ZSSF, Mohamed Fakih Mzee,  ambapo alisema kuwa mwanachama anapostaafu hupewa mafao yake yote kwa mujibu wa sheria.

Alisema mafao ya kiinua mgongo ya mwanachama anayestaafu hupewa kwa ajili ya kulipwa pensheni ya kila mwezi, kama baadhi ya watu wanavyodai.

“Hakuna mafao ya mwanachama yanayobakishwa kwa ajili ya kulipwa pensheni, mafao yake yote ya kiinua mgongo hupewa mwanachama mwenyewe,” alisema.

Akiwasilisha mada ya mabadiliko ya sheria ya ZSSF, Mzee alisema pamoja na mapendekezo ya mabadiliko yaliyotolewa kuleta athari za kijamii, kisiasa na kimapato kwa wanachama, lakini bado ZSSF itaendelea na shughuli zake zilizokusudiwa.

“Mapendekezo yenyewe ni kuongeza viwango vya uchangiaji kutoka asilimia 15 hadi 20 kwa uwiano wa 13.7, kuongeza muda wa kuchangia ili kustahiki kupata mafao ya uzeeni kutoka miezi 60 hadi miezi156, kubadili fomula ya ukokotoaji wa mafao, mfuko kubaki katika mfuko wa DB badala ya CD na umri wa kustaafu kubaki miaka 60,” alisema.

Naye Meneja wa ZSSF Kanda ya Pemba, Rashid Mohamed Abdalla, alisema fedha alizochangia mwanachama kwenye mfuko huo hazipunguzwi kati ya kile alichochangia.

Akizungumzia suala la kujichangia kwa hiari, Ofisa Uhusiano kutoka ZSSF,  Mussa Yussuf, alisema lengo la kuanzishwa mfuko huo ni kuwaingiza walio nje ya mfumo rasmi wa ajira ili kuwapatia wananchi haki ya hifadhi ya jamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles