26 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

ZELOTE: RAIS NDIYE ATAKAYENIONDOA MADARAKANI

Na Gurian Adolf-Sumbawanga


MKUU wa Mkoa wa Rukwa, Zelote Steven amewaambia wafugaji mkoani humo mwenye uwezo wakumuondoa ni Rais pekee, kwani ndiye aliyempangia akafanye kazi na wala sio wao.

Akizungumza wakati wa kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika hivi karibuni, alisema wapo baadhi ya wafugaji wanaomchukia kiasi cha kutaka aondoke kwakua amekuwa akiwakamata pindi wanapo kiuka utaratibu wakusafirisha mifugo yao kwani wengine huipitisha kwenye barabara za lami.

Alisema mara nyingi amekuwa akiwazuia wafugaji kuingiza mifugo yao mkoani humo na wakati mwingine kuwakamata yeye mwenyewe kitendo kinachowaudhi nakuona Kama anawanyanyasa.

“Baadhi ya wafugaji nimekuwa nikiwakamata mwenyewe na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria, wanakiuka utaratibu unaowataka kusafirisha mifugo yao kwa kutumia malori, wamekuwa wakikaidi na ninapo wakamata wanaweka chuki kiasi kwamba wanauliza nitaondoka lini”alisema

Alisema hakuna mwenye uwezo wa kumuhamisha Mkoa wa Rukwa ama kutengua nafasi hiyo labda Rais  Dk. John Magufuli, lakini wao wasahau wanachopaswa kufanya ni kutiisheria kwani hawezi kuwavumilia kwakuwaacha wapitishe mifugo katika barabara za lami zilizojengwa kwa gharama kubwa.

Naye  Mbunge wa Kwela,  Ignas Malocha (CCM),  aliutaka uongozi wa mkoa huo kukabiliana na ma wakala  wa pembejeo za kilimo ambao wamekuwa na tabia ya kuwauzia wakulima pembejeo za bandia.

Alisema baadhi ya wakulima wamekuwa wakipata hasara kwa kununua pembejeo za bandia na hivyo kuzidi kuwatia umasikini.

“Hivi sasa karibu tunaanza msimu wa kilimo, ni vizuri serikali ya mkoa ikaanza kujipanga kuwadhibiti mawakala hao ili kuwalinda wakulima wasipate hasara,”alisema.

Aliwasihi wakulima kuendelea kujituma katika kilimo licha ya malalamiko ya bei ya mazao kuwa ya chini kwani itafika wakati watanufaika na kilimo cha muhimu ni kuto kukata tamaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles