Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital
TIMU ya soka ya wasichana ya Zanzibar wenye umri chini ya miaka 18, imeanza vibaya mashindano ya CECAFA kwa kufungwa na Uganda mabao 3 -0 katika mchezo uliopigwa leo Julai 27, 2023 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mabao yote ya Uganda yalifungwa kipindi cha pili Patricia Nanyazi, Agnes Nabukenya, Phionah Nabulime.
Akizungumzia matokeo hayo, kocha wa Zanzibar, Abdulmutik Haji, amesema kipindi cha kwanza walianza vizuri na kwenda mapumziko bila kuruhusu bao.
Alieleza kuwa pamoja na timu yake kucheza vizuri lakini kipindi cha pili walishindwa kupiga pasi za mwisho kutokana na kudhibitiwa na wapinzani.
Amesema tatizo hilo ameliona na anakwenda kulifanyia kazi kabla ya kukutana na Tanzania Bara, Julai 30, 2023.