26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

YAFAHAMU MATUNDA MATANO YENYE UZITO MKUBWA KULIKO DUNIANI

Kila uchao ulimwengu huwa haukosi maajabu na raha zaidi ni pale panapopatikana vitu vyenye utofauti lakini pia kufikia hatua ya kuingia katika kumbukumbu za dunia kwa upekee wake.

Katika kumbukumbu hizo yapo matunda pia ambayo yamekuwa ni gumzo kwa wengi kwa utofauti wake ukilinganisha na mengine, jambo linaloyafanya kuwa kivutio kikubwa kwa watu.

Yafuatayo ni baadhi ya matunda ambayo yamefanikiwa kuingia katika kumbukumbu hizo za dunia;

pmpkinBoga: Hili lina sifa za kipee lina uzito wa kilo 1056, limelimwa na binadamu huko mjini Atlantic, Marekani na sio kujitokea porini.

Kwa muonekano, lina umbo kubwa na linashangaza kila alionae. Limekuwa kivutio kikubwa kwa wengi kwa namna lisivyo la kawaida.

lemonLimao: Tunda hili kidunia lina uzito wa kilo 5.265 na urefu wa sentimeta 74, limelimwa na Aharon Shemoel katika shamba lake huko Kefar Zeitim, Israel.

heaviest-appleApple: Ni yale ya rangi nyekundu na laini, lina uzito wa 1.849 ambazo ni sawa pauni 4. Limepatikana katika shamba la bwana Chisato Iwasaki katika shamba lake lililopo mji wa Hirosaki, Japan.

swt-potatoKiazi kitamu: Mkulima wa Lebanoni, Khalil Semhat, kutoka mji wa Tyre kusini, hakuamini baada yakuona kiazi kikubwa sana kutoka katika shamba lake, kina kilo 11.3 na hii ikakifanya kiazi hicho kuwa ni kiazi kikubwa kuliko vyote duniani.

a422_watermellonTikitimaji: Kidunia tunda hili limeshika nafasi ya kwanza kwa ukubwa wake kama tikitimaji. Lina uzito wa kilo 122.Lloyd Bright, katika ukulima wake wa matikiti maji hakuwahi kupata tunda kubwa kama hilo kwa miaka mingi sana hivyo hata yeye ameshangazwa na tunda hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles