30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

WHI yawaita Watanzania kuwekeza mfuko wa Faida Fund

*Yasema hauna hatari ya aina yoyote
*Mwekezaji kupata faida kulingana na uwekezaji wake
*Umepewa msamaha wa kodi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Watumishi Housing Investment(WHI) ni Taasisi ya umma chini ya Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Mbali na kujenga nyumba kwenye maeneo mbalimbali ambazo zimekuwa zikiuzwa na nyingine kupangishwa, WHI kwa sasa imeanzisha mfuko wa Faida Fund.

David Mwaipaja ni Afisa Masoko wa WHI, ambapo anafafanua kuwa mfuko huo ni mpango ulio wazi unaotoa fursa nyingine ya uwekezji kwa Watanzania hasa wa kipato cha chini.

“Hii ni kupitia uwekezaji katika vipande ili kupata mapato shindani kupitia ukuaji wa mitaji na kutengeneza utamaduni wa kuwekeza katika masoko ya fedha na mitaji,” anasema Mwaipaja.

Moja ya majengo ya mradi wa Watumishi Housing Investment(WHI) katika eneo la Gezaolole, Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Anasema kuna sababu nyingi za kuwekeza kwenye mfuko wa Faida Fund.

“Kwanza kabisa mfuko unaendeshwa na wataalamu waliothibitishwa na mamlaka ya mitaji na masoko(CMSA), pia kulinda mtaji, hatari ndogo za uwekezaji wa kiwango kikubwa cha ukwasi ni sifa ya uhakika wa mfuko huu,” anasema Mwaipaja na kuongeza kuwa.

“Mfuko umelenga kufanya uwekezaji katika maeneo yenye kutoa athari ndogo za uwekezaji na wenye kukidhi mahitaji ya mwekezaji kwa haraka.

“Pia uwekezaji wenye kutoza viwango maalum vya riba katika kipindi kisichopungua mwaka mmoja kama vile hati fungani za serikali, dhamana za serikali, akiba maalum katika mabenki, dhamana za mashirika zilizoorodheshwa katika soko la mitaji,” anasema Mwaipaja.

Nani anaruhusiwa kuwekeza?

Mwaipaja anasema kuwa mfuko huo uko wazi kwa Watanzania ni na wakazi waliopo ndani na nje ya nchi, unahusisha watu binafasi (ikijumhisha watoto) na wawekezaji wasio watu binafsi kama mifuko ya pensheni, mabenki/mashirika, taasisi za serikali, mamlaka za udhibiti, vyombo vya ulinzi na usalama na asasi zisizo za kiserikali na mashirika mengine.

Kiwango cha Uwekezaji

Anasema kiwango cha awali cha uwekezaji ni kuanzia Sh 10,000.

“Mauzo yanayofuata baada ya yale ya awali ni Sh 5,000, kumbuka kuwa hakuna kiwango cha juu cha uwekezaji.

“Fedha hizo zitawekezwa kwenye masoko ya fedha na mitaji yenye kiwango cha chini cha hatari za uwekezaji,” anasema.

Akifafanua zaidi kuhusu tozo ya kujiunga Mwaipaja anasema kuwa mwekezaji hatotozwa gharama yoyote ya kujiunga au kujitoa katika mfuko.

“Baada yab kipindi cha utulivu kumalizika, uuzaji wa vipande utafanyika kila siku, mfuko utatuma malipo ya mauzo ya vipande ndani ya siku tatu za kazi baada ya kupokea maombi.

“Katika makao makuu ya WHI fedha za mauzo zitatumwa moja kwa moja katika akaunti ya benki ya mwekezaji. Pia kwa mujibu wa sheria za nchi mgawanyo wa mapato ya mfuko yamesamehewa kodi ya mapato kwa wawekezaji,” amesema Mwaipaja.

Watumishi Housing Investment wapo katika maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama sabasaba wakiwa katika jengo la Karume hivyo wamewakaribisha Watanzania kutembelea banda hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles