MONROVIA, LIBERIA
NYOTA wa zamani wa mpira wa miguu, George Weah na Makamu wa Rais Joseph Boake, wanaelekea duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Liberia.
Karibu matokeo yote ya uchaguzi huo uliofanyika Jumanne iliyopita yameshahesabiwa, kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi.
Weah ambaye ni mwafrika wa kwanza kushinda tuzo ya mwanasoka bora wa FIFA wa dunia, ameongoza uchaguzi huo kwa asilimia 39 huku Boakai akiwa wa pili kwa asilimia 29.
Duru ya pili kati ya wawili hao wanaowaongoza wagombea wengine 20 kuwania kumrithi mwanamke wa kwanza kuwa Rais barani Afrika, Ellen Johnson Sirleaf, ambaye pia ni mshindi wa tuzo la amani la Nobel itafanyika mwezi ujao.
Weah (61) anaungwa mkono kisiasa na Rais wa zamani wa taifa hili aliye jela, Charles Taylor na mgombea wake mwenza Jiwel Howard ni mke wa bwana vita huyo.
Joakai (73) amepewa jina la utani la ‘Sleepy Joe’ akimanisha Joe msinziaji kwa vile mara nyingi camera humkuta akisinzia, lakini mwenyewe amelikana jina hilo.
Aidha anasema amejitenga na rekodi ya Sirleaf akisema mengi yanahitaji kufanywa.