26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Watumishi GST  watakiwa kudumisha ushirikiano

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Dk. Mussa Budeba ameongoza Kikao cha Baraza la Wafanyakazi la taasisi hiyo na kuwata watumishi hao kudumisha ushirikiano.

Kikao hicho kimefanyika Januari 14, 2024 katika ukumbi wa Profesa. Abdulkarim Mruma jijini Dodoma.

Akifungua Mkutano huo, Dk. Budeba amewaasa watumishi kuwa wawazi na kutumia fursa hiyo kuwasilisha na kujadili hoja muhimu zitakazofanya uboreshaji na ufanisi wa majukumu ya taasisi hiyo.

“Kila mtumishi azungumze hoja kwa uwazi bila kuwa na hofu kwa lengo la kuboresha utendaji kazi katika maeneo yetu ili kuleta umoja, upendo na mshikamano hususan katika kipindi hiki cha Vision 2030, Madini ni Maisha na Utajiri,”amesema Dk. Budeba.

Naye Mchumi Mkuu wa GST,  Lameck Kajala, amewasilisha mada ya mapito na mchanganuo wa bajeti ulioidhinishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka 2023/24 na Rasimu ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/25.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Wafanyakazi Mkoa wa Dodoma (TUGHE),  Samwel Nyungwa amesema Baraza la wafanyakazi lipo kwa mujibu wa Sheria ambalo ni agizo la Rais Na. 1 la mwaka 1970, kazi zake ni pamoja na kuishauri Serikali katika shughuli zake na kuhakikisha watumishi wa  wanashirikishwa kwenye shughuli za kiserikali.

Katika Mkutano huo watumishi na wajumbe wote wamepata fursa ya kujadili  utejelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo ikiwa ni pamoja na kujadili na kupitisha Rasimu ya Bajeti kwa mwaka wa fedha 2024/25 kwa manufaa ya taasisi hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles