26.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 23, 2024

Contact us: [email protected]

Watu 40 waambukizwa corona kwa kuhudhuria ibada

 FRANKFURT, UJERUMANI

TAKRIBAN watu 40 wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya corona baada ya kuhudhuria ibada kanisani katika mji wa Frankfurt.

Idara ya afya katika mji huo imesema mtu mmoja kati ya hao 40 ndiye yuko hospitalini ilhali wengine sio wagonjwa.

Wakati huo huo mamlaka katika mji jirani wa Hanau ulio Mashariki mwa Jiji la Frankfurt imesema watu wapatao 16 kutoka mji huo wameambukizwa na virusi vya corona baada ya kuhudhuria ibada ya kanisani mjini Frankfurt.

Ili kuzuia maambukizi zaidi, mamlaka ya mji huo wa Hanau imefutilia mbali hafla nyengine iliyokuwa imepangwa kufanyika jana Jumapili katika mji huo.

WALIOAMBUKIZWA AFRIKA WAPINDUKIA 100,000 

Wakati huo huo, takwimu za hivi karibuni za Kituo cha Kinga na Udhibiti wa Magonjwa cha Afrika (Africa CDC) zinaonyesha kuwa, idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona barani Afrika imezidi 100,000.

Kwa mujibu wa taarifa ya Africa CDC hadi kufikia Jumamosi Mei 23, kesi zilizothibitishwa rasmi za corona au Covid-19 barani Afrika ni 103,933. Aidha jumla ya waliofariki kutokana na Covid-19 barani Afrika ni 3,183 huku waliopona baada ya kupata matibabu wakiwa ni 41,576.

Kituo cha Africa CDC kimeongeza kuwa hadi sasa virusi vya corona vimesambaa kwenye nchi zote za Afrika, na eneo la Kaskazini mwa Afrika limeathirika zaidi.

Mkurugenzi wa WHO barani Afrika Daktari Matshidiso Moeti alisema kwa sasa janga la Covid-19 halijaibua maafa makubwa Afrika kwani idadi ya waliofariki ni ndogo ikilikanishwa na maeneo mengine duniani.

 Hata hivyo WHO inasema idadi ya waliopimwa Covid-19 barani Afrika ni ndogo kwani hadi sasa kumekuwa na vipimo milioni 1.5 tu na kwa msingi huo nchi nyingi zinahitaji msaada kuongeza idadi ya vipimo. 

Afrika Kusini yenye kesi 18,000 za Covid-19 ndiyo nchi yenye idadi kubwa zaidi ya maambukizi barani Afrika.

WATOTO MILIONI 80 WAKOSA CHANJO

Katika hatua nyingine Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema kuwa janga la corona limevuruga mpango wa utoaji wa chanjo za magonjwa ya kupooza (polio), surua na kipindupindu kwa makumi ya mamilioni ya watoto duniani.

Katika ripoti yake mpya ya mwishoni mwa wiki, WHO ilisema watoto karibu milioni 80 wenye chini ya umri wa mwaka mmoja wapo katika hatari ya kupoteza maisha iwapo watakosa chanjo hizo.

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema katika taarifa kuwa, “kukatizwa utoaji wa chanjo kutokana na janga la Covid-19 kunahatarisha kusambaratisha mafanikio yaliyopatikana ndani ya miongo kadhaa iliyopita, katika kukabiliana na magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa chanjo kama vile surua.”

 Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa UNICEF umesema kusimamishwa safari za ndege na kuwekwa sheria kali za kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19 (Corona) kumepelekea kusimama kwa sughuli za ufikishaji na utoaji wa chanjo katika nchi zinazohitaji hususan za Kiafrika.

Inaarifiwa kuwa, kampeni 46 za utoaji wa chanjo ya kupooza kwa watoto zimesimamishwa katika nchi 38 duniani hususan za Afrika, baada ya nchi hizo kusimamisha safari zake za ndege ili kuzuia ueneaji wa corona.

WHO Mei mwaka jana lilitangaza huko nyuma kuwa, huenda likatangaza karibuni hivi kuwa bara Afrika halina tena ugonjwa wa kupooza wa Polio. Awali bara hilo lilikuwa limeanzia kuutokomeza ugonjwa huo kufikia mwaka 2000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles