Watumishi watakaobainika kujihushisha na shughuli za uchimbaji madini katika eneo la misitu ya Amani iliyopo wilayani Museza mkoani Tanga, watachukuliwa hatua kali ikiwamo kufukuzwa kazi au kufungwa jela.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella leo wakati alipokuwa kwenye ziara maalumu ya kujionea uharibifu wa mazingira unaofanywa na wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu katika eneo la Mto Zigi uliopo ndani ya hifadhi ya msitu huo.
“Kumekuwa na malalamiko ya wananchi kwamba wapo baadhi ya watumishi wanaojihusisha na uchimbaji wa madini katika vyanzo hivi vya maji, sasa niwaambie tu jambo yeyote atakayebainika adhabu yake ndiyo hiyo.
“Uharibifu unaofanywa hapa unatishia usalama wa vyanzo vya maji katika Jiji la Tanga ambapo wakazi wake hutegemea maji kutokakatika chanzo cha Mto Zigi,” amesema Shigella.
Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa pia alizindua jumuiya za watumiaji maji pamoja na mradi wa maji katika vijiji vya Mashewa, Kimbo na Shembekeza.