25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

‘WANAWAKE MIGODINI HUZUIWA KUNYONYESHA WATOTO’

Na SHOMARI BINDA-MWANZA

OFISA Uhamasishaji Chama cha Wafanyakazi wa Tasnia ya Migodi na Nishati Tanzania (NUMET), Aloyce Shigela, amedai asilimia kubwa ya wanawake wanaofanya kazi migodini, wamekuwa wakikosa fursa ya kuwanyonyesha kwa wakati watoto wao pale wanapojifungua kutokana na kubanwa na waajiri wao kwenye maeneo ya kazi.

Akizungumzia miaka sita ya NUMET, Shigela, alisema wafanyakazi wanawake wamekuwa wakishindwa kufanya hivyo kutokana na mazingira yao ya kazi na kubainisha kuwa wapo wanaofukuzwa kazi pale wanapokuwa na ujauzito na wale wanaobaki kazini baada ya kujifungua wao wamekuwa hawapati muda wa kutosha kuweza kunyonyesha watoto hali inayodhoofisha ukuaji wa mtoto.

Alisema waajiri wengi katika maeneo ya migodi, wamekuwa wakiwachukulia mwanamke kama watu walioshindwa kufanya kazi wanaopata ujauzito jambo ambalo si kweli na linapoteza haki zao.

Alisema mwanamke anapaswa kupata muda wa kutosha kunyonyesha pale anapojifungua ili anyonyeshe mtoto akue na awe na afya njema hivyo kutoa wito kwa wahanga kutoa taarifa pale wanapokutana na matukio ya namna hiyo.

“Numet ni chama cha kipekee ambacho kimekuja kuwasaidia wafanyakazi wanaofanya kazi katika maeneo ya migodini na kwenye nishati ikiwemo suala pia la kumjali mwanamke hususani pale anapokuwa amejifungua kupata haki ya kumnyonyesha mtoto kwa muda unaostahili.

“Waajiri kwenye migodi ni watu ambao wakati wote wanataka faida, lakini zipo haki za wafanyakazi ambazo wanaziminya na wafanyakazi kwa kutokujua sheria wanakaa kimya huku wakiendelea kuumia jambo ambalo halifai,” alisema Shigela.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Taifa wa chama hicho, Nicomedes Kajungu, alisema kukata tamaa kwa wafanyakazi wengi wa tasnia hiyo kutokana na manyanyaso kutoka kwa waajiri wanapojiunga na vyama vya wafanyakazi kwani imekuwa changamoto kubwa.

Alidai wafanyakazi wengi hususani kwenye maeneo ya migodini hawana mikataba hivyo kuwa na wasiwasi wa kujiunga wakiogopa kufukuzwa kazi jambo ambalo linawapotezea haki zao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles