Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM
WITO umetolewa kwa wanaume kuhakikisha wanawasindikiza wake zao kliniki kama njia ya kujenga upendo wakati wote na baada ya kujifungua.
Hatua hiyo imetajwa kusaidia kujenga furaha kwa mama mjamzito ikiwa ni pamoja na kujifungua mtoto mwenye afya.
Hayo yalisema juzi mjini hapana Padri Festus Makwame wa Kanisa Katoliki Mtakatifu Tereza Jimbo la Arusha alipokuwa kwenye ibada ya mkesha wa Sikukuu ya Krismas ambapo alisema wanaume wengi hawapo karibu na wake zao pindi wanapokuwa wajawazito jambo ambalo ni kosa kubwa kwa Mungu.
“Wanaume wasindikizeni wake zenu kliniki huoni kwamba unashirikiana na Mungu katika uumbaji tena anakujengea heshima ya wewe kuitwa baba fulani?
“Nenda naye yapo mambo mengi mtakayoelekezwa hata namna ya vyakula anavyotakiwa kula akisahau kwa vile ulikuwepo utamkumbusha. Hebu igeni mfano wa Joseph na Maria hadi Yesu Kristo anazaliwa walikuwa pamoja.
“Wacha tuwe wakweli hakuna jambo gumu kama kumsamehe mtu aliyekukosea tena kwa makusudi, lakini kwa vile Mungu ameagiza tusameheane ni lazima tufanye hivyo na ukweli utabakia kuwa hivi msamaha wa kweli ni ule ambao unautoa huku unauma umekosewa lakini unasamehe kwa faida yako mwenyewe,” alisema.