Na Renatha Kipaka, Bukoba
BAADHI ya wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAÂF) wa Manispaa ya BukÂoba mkoani Kagera wameiomba Serikali kueÂndelea kuwaingiza kwÂenye mpango wa awamu pili ili waweze kujÂiimalisha katika mirÂadi yao na kuondoka na utegemezi.
Wakizungumza na Mtanzania Digital leo wanufaika hao wamesema wamefanikiwa kuanzisha vitu mbalimbali ambavyo vinazalisha pesa kutokana na ruzuku waÂnayopokea​ kupitia mpango huo.
Mkazi wa Mtaa wa KisÂindi kata Kashai ManÂispaa ya Bukoba, CefrÂoza Rugaiyamu amesema, kabla hajaingizwa kwenye mpango huo wa kuÂnusuru kaya maskini maisha yake yalitegeÂmea huruma za majiraÂni.
“Mimi na wajukuu zanÂgu tumeiishi kwa kunÂywa uji mchana na jiÂoni ambao tulipewa na majirani sina nguvu za kutafuta mahitaÂji ya wajukuu watatu ambao ninaishi nao kama malezi.
“Nilipopata pesa Sh 24,000 kila dirisha niliÂkuwa natunza kidogo hadi nimefikia hatua ya kufungua genge la ndizi mkaa na nyanÂya, mjukuu wangu ndiye anae uza genge hili na limekuwa na msaada mkubwa kwangu,” amesema.
Mkazi wa kata Nyanga, Devotha Kanura amesema awali aliishi kweÂnye chumba kimoja yeÂye na familia yake kÂwa miaka sita taÂngu TASAF imemtabua ameweza kujenga nyumba ya vyumba vitatu na kuanzisha mradi wa ufugaji.
“Kwa kipindi hicho nimetumia kubadilisha maisha kidogo ya chumba kimoja hadi kujenga vyumba vitatu na kufuga bata pamoja na nguruwe ambao wananisaidia kuongeza kipatoÂ,” amesema Kanura.
Amesema bado msaada zaidi unahitajÂika kwani mategemeo ni kusimama wenyewe na kuendeleza miradi na kuondokana na kutegÂemea misaada.
Mratibu wa mpango wa kunusuru kaya maskiÂni mkoani Kagera, EfrÂaz Mkama amesema jukÂumu la wanufaika ni kutambua kuwa miradi ya (TASAF) sio ya kudumu na enÂdelevu lazima kuweka akiba kwa kuanzisha miradi ambayo itakuwa ni endelevu itakuwa endelevu.
“Endapo mpango utafiÂkia mwisho wao wabaki na shughuli ambayo itaendelea kama TASÂAF namanisha kujiinua katika uchumi kupiÂtia miradi yao,” amesema Mkama.
Ameongeza kuwa Mkoa wa KageÂra umetekeleza kwa miaka sita na kujikita katika utoaji wa fedha, uanzishaji wa vikundi vya kilimo, uÂfugaji na ujasiriamaÂli na kujenga uwezo wa kuongeza kipato.
Ameongeza kuwa kaya zilizofikiwa ni 5,66Â03 sawa na vijiji 471 amÂbazo zililipwa Sh biÂlioni 61.1na vikundi 485 vilitambuliwa ndÂani na kuwekeza Sh mÂilioni 23.8 kwa ajili ya kuongeza kipato.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mpango wa kunusÂuru kaya maskini, OscÂar Maduhu​ amesema mpango huo wa pili awamu ya tatu umejikita kwenye nguvu kazi, kulipwa ujira kwa ajili ya kuÂongeza kipato na kukÂuza uchumi.
Hata hivyo aamesema kaya milioni 1.4 ambazo hazikuweza kuiÂngizwa kwenye kipinÂdi cha kwanza vitaonÂgezwa kwa kutumia mfÂumo wa kieletroniki kutoka mfumo wa awali kupokea fedha mkononi.