25.5 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

WANAFUNZI WENGI HAWAJUI KUANDIKA CV

Na JOSEPH LINO


WANAFUNZI wengi hawajui nini cha kuandika kwenye wasifu (CV) kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza masomo ya Chuo Kikuu. Wengi hawajui waandike nini au vitu ambavyo havipaswi kuwepo kwenye CV.

Kuandika CV kwa mara yako ya kwanza ni mchakato ambao unaweza kukuondolea kujiamini.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya ajira za mtandao ya  The Ladders, umebainisha kuwa waajiri wengi hutumia wastani wa sekunde sita kuangalia CV kabla hawajafanya maamuzi ya kuchukua mtu sahihi.

Mtaalamu wa Taaluma wa  The Ladders, Amanda Augustine anasema hakuna sheria ngumu ya kuandika CV, inategemea kile ambacho unapaswa kuandika ni kile unaweza kufanya katika kazi, kuna miongozo ya awali ya wanafunzi au wataalamu waliomaliza masomo na hawana uzoefu.

“Kuwepo katika soko la ajira baada ya chuo kikuu ni jambo la furaha na  la kusisimua. Lakini wahitimu wengi wanajikuta kwenye changamoto ya kuhitaji uzoefu wa kupata kazi, unahitaji kazi ili kupata uzoefu,” anasema.

 

Kwa bahati nzuri, ujuzi ambao waajiri huthamini zaidi haupatikani tu katika ulimwengu wa ajira bali mbinu za kuandika CV bila kuwa na uzoefu wa kazi. Namna unayoandika CV yako  kwa njia ya ubunifu zinaweza kuonyesha ujuzi unaoweza kuhamasisha mwajiri kuwa wewe ni bora.

 

 Namna ya kuandika CV bila kutaja uzoefu wa kazi;

Tambua sifa zako muhimu

Kuandika CV kimsingi ni kuweka katika hali ya kujiuza kibinafsi. Kitu cha kwanza ni kujua au kuwa na kielelezo cha kitu unachokiuza, tengeneza orodha ya vitu vyote unavyoweza kufanya bila kujali kama una sifa za kitaaluma au hapana. Kisha, linganisha orodha ya sifa za waajiri wanaotafuta.

 

Anza na maelezo binafsi

Hiki ni kitu cha kwanza kabisa mwajiri yeyote anaanza kusoma, hivyo andika kwa makini. Maelezo yanahitaji kuwa mafupi iwezekanavyo wastani wa maneno 150.

 

Anza kwa kujitambulisha kwa kiwango chako cha elimu na ujuzi wako mfano (“Mimi hufanya kazi kwa juhudi kubwa na mwenye kujitegemea ambaye nimehitimu hivi karibuni.

 

Hivyo uongeze kwa kuweka shahada uliyosomea au chuo kikuu kama unahisi ni muhimu kulingana na jukumu la kazi unaloomba.

 

Hakikisha unataja moja kwa moja kazi unayoombwa au taja kazi unayotafuta lakini pia weka chaguo lako wazi kwa ujumla.

 

Taja ujuzi wako badala ya majukumu

CV nyingi huanza kwa kuweka orodha ya ajira ambazo umefanya hivi karibuni, lakini kama hujafanya kazi kabla au umefanya kazi katika sekta isiyo rasmi, ni vyema zaidi kuanza CV yako na orodha ya ujuzi uliyoipata. Waajiri watawaona kuwa CV yako ya kuvutia zaidi na muhimu zaidi.

 

Usisahau ujuzi wa kawaida

Je! una leseni ya dereva? Je, unaweza kutumia programu mbalimbali za kompyuta? Je, wewe uelewa wako wa mitandao ya kijamii? Mara nyingi, wahitimu wengi huacha ujuzi ambao waajiri wanataka kwa sababu wanafikiri kuwa si muhimu.

 

Ikiwa unaweza kufanya kitu ambacho kinaweza kuwa na manufaa kwenye sehemu ya kazi, hasa utumiaji wa programu za kompyuta, lugha ambazo unaweza kuzungumza (hutahitaji mzoefu wa kuongea lugha fulani ila ni muhimu, pia usidanganye uwezo wako kwa kila jambo.

Inaendelea wiki ijayo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles